Waziri wa Uchukuzi,Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyevaa tai nyekundu),akimtambulisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (aliyenyoosha mikono)Mhandisi Madeni Kipande,mchana huu alipotembelea Bandari hiyo.Waziri wa Uchukuzi wa Uchukuzi amewasimamisha Maneja wa Bandari ya Dar es Salaam,Meneja wa Kurasini Oil Jet(KOJ),Meneja wa JET,Mhandisi wa kituo cha Mafuta(Oil Terminal Engineer),Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari(TPA),na Wakurugenzi Wakuu Wasaidizi wawili wa Mamlaka hiyo kupisha Uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinzoikabili Mamlaka hiyo.
Waziri wa Uchukuzi,Harison Mwakyembe(aliyesimama) akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA),mchana huu,wakati akiwataka kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao.
Sehemu ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA)wakimsikiliza Waziri wa Uchukuzi,hayupo Pichani,wakati alipowatembelea leo mchana na kuwaeleza dhamira yake ya kuongeza ufanisi katika utendaji wa Mamlaka hiyo.
Ndiyo Mzee fagia tunataka usafi kila mahali, tunaomba tu ufagie takataka na usifagie na shilingi yetu tafadhali.
ReplyDeleteMlolongo Uko hivi: Mawaziri kadhaa wanatuhumiwa kwa ufisadi na kutokuwa makini(unakumbuka kiwanja alichouziwa Mohamed Entreprises na madudu ya TANESCO?)---Wabunge wanachachamaa, Zitto anakusanya saini za wabunge kupiga kura ya kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu na ajiuzulu au amshauri Rais awawajibishe mawaziri----Waziri Mkuu hajiuzulu, Raisi analazimika kuwafukuza mawaziri na kurekebisha baraza la mawaziri---Anapowatangaza wapya anasema walioondoka wasiende peke yao, bali na wakurugezi/wakuu wa Idara na Mashirika walioharibu kazi pia waondoke----wanaondolewa Uchukuzi, Nishati na Madini, Maliasili na Utalii---na leo bandari!. Maagizo ya Rais yakitekelezwa tutasogea!
ReplyDeleteHuyu Mheshimiwa, ni MKONO wa Mwenyezi Mungu wa kuinusuru Tanzania kuendelea kupata madhara ya ufisadi. Yaliyokuwa yanafanyika hapo bandarini, yalihitaji guts kama za Mwakyembe kuyafichua. Uzuri ni kuwa hata huko bandarini kwenyewe staff walishachoka, hivyo alichokifanya huyu Mheshimiwa ni kukusanya taarifa toka kwao na kuamua kuzifanyia kweli!!!
ReplyDeleteUkipata muda, soma blogs nyingine uone jinsi ambavyo utajiri wa kina Mgawe umeshaanza kuanikwa!!!! Jamani, watu wachache wanaishi kwenye UTUKUFU hapa hapa duniani kwa gharama ya watanzania wengi wanaoteseka kila uchao. Hivi laana ya hao watanzania maskini itawaponesha hao walafi kweli???
Nasikia kuna kigogo mmoja huko Uchukuzi, ambaye afya yake ilianza kuwa mgogoro mara tu Mwakyembe alipoteuliwa kuwa Waziri wa Uchukuzi. Huyo kigogo wanasema kafa kwa presha hivi majuzi tu!!! Kwa mwendo huu wa Mwakyembe, wataondoka wengi! Hongera sana Mheshimiwa. Amini kuwa zaidi ya asilimia 90 ya watanzania wanakuombea dua, ili usidhurike tena kama awali.