Mhandisi wa Airtel mkoani Iringa bw
Joshua Kadege akitoa ufafafanuzi kwa mwenyekiti wa kijiji cha Kimande tarafa ya
Pawaga-Jimbo la Isimani bw Anderson Mpululu jinsi mtambo wa mawasiliano
uliowekwa na Airtel kijiji hapo unavyofanya kazi ili kurahisisha mawasiliano
katika kijiji hicho.Airtel imeanza kufunga mitambo ya mawasiliano itakayotumia
nguvu za Nishati ya jua (solar) ili kufikisha mawasiliano katika
maeneo ya vijijini, kati ni meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania bw Jackson
Mmbando wakati wa hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika kijijini Kimande nje ya
mji wa Iringa jana.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania
akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Kimande tarafa ya Pawaga-Jimbo
la Isimani bw Anderson Mpululu kuhakikisha wanaweka ulinzi shirikishi kulinda
mtambo mpya wa mawasiliano unaotumia nishati ya jua uliowekwa na Airtel ili
kufikisha huduma bora ya mawasiliano kijijini hapo, wakwanza kulia
ni Meneja Mauzo wa Airtel Nyanda za juu kusini Bw, Beda Kinunda na
kushoto ni Injinia wa Airtel mkoani Iringa bw Joshua Kadege. Hafla ya uzinduzi
ilifanyika kijijini Kimande nje ya mji wa Iringa jana.
Kulia ni Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando na bw Beda Kinunda
Meneja wa Mauzo wa airtel Mkoani Iringa wakiwa nje ya Mnara wa
Airtel unaotumia nguvu ya Nishati ya jua (solar) wakizungumza na
Mwenyekiti wa kijiji cha Pawaga-Jimbo la Isimani bw Anderson Mpululu
(shoto) mara baada ya Airtel kuzindua rasmi mnara wa mawasiliano unaotumia
nguvu za Solar katika kijiji cha Kimande tarafa ya Pawaga-Jimbo la Isimani,
Airtel imezindua mnara huo unaotumia nishati ya jua kwa lengo la kufikisha
mawasiliano katika maeneo ya vijiji ambapo bado hakujafikiwa na umeme wa taifa
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
inayoongoza kwa kutoa huduma zenye wigo mpana zaidi imezindua minara yake
inayotumia Umeme unao tumia nguvu za nishati ya Jua katika kijiji cha
kimande kata ya itunguru mkoani Iringa. Uzinduzi huo ni moja kati ya
mikakati ya Airtel kuhakikisha inaendeleza mipango yake ya kupanua upatikanaji
wa mawasiliano katika maeneo mbalimbali nchini kirahisi, kupunguza gharama za
uendeshaji na kuhamasisha utunzaji wa mazingira katika maeneo yenye minara yake
nchini.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo
Mwenyekiti wa kijiji cha Kimande kata ya Itunungu Tarafa ya Pawaga Iringa
Vijijini Bw, Andason Mpululu ameushukuuru uongozi wa Airtel kwa kuweza kukabili
changamoto za mawasiliano kijijini hapo na kuwa sehemu ya uboreshaji wa
uendeshaji wa biashara mbalimbali hasa za kilimo cha mpunga ambapo hapo awali
upatikanaji wa soko ulikuwa mgumu sana kutokana na kutokua na mawasiliano
thabiti kama ilivyo sasa.
“Kwa kupitia Mtandao na huduma ya
Airtel money huduma za kifedha zimeboreshwa, zimekua karibu zaidi na
kuwawezesha wafanyabiashara kupokea malipo ya bidhaa zao kirahisi, kwa gharama
nafuu na bila usumbufu wowote. Nimatumaini yetu kuwa kwa kupitia umeme wa sola
gharama za mawasiliano ya simu za mkononi yataaendelea kupungua na kuboreshwa
zaidi na kuleta tija kwa wananchi hasa wenye kipato kidogo” alisema bwa Mpululu
Naye mkazi wa kata ya Itunungu bwana
Jumanne Zuberi alisema “tunashukuru sana serikali kuwawezesha wawekezaji
kuwekeza katika sekta ya mawasiliano na hivyo kufikiwa na mtandao wa Airtel.
Hapo zamani upatikanaji wa mawasiliano ulikuwa ni changamoto kubwa hivyo kuwafanya
wakazi wa kijiji hapa kutembea umbali mrefu kupata mawasiliano. Tunashukuru kwa
sasa huduma za simu kijini hapa zimeweza kuboresha shughuli mbalimbali za
kiuchumi, kijamii na kuboresha usalama wa raia na mali zetu”.
Akiongea kwa niaba ya kampuni ya simu
za mkononi ya Airtel Meneja Uhusiano bw, Jackson Mmbando alisema” nia yetu ni
kubadili matumizi ya mafuta ya diesel na generator kuendesha mitambo yetu ya
mawasiliano na kutumia umeme wa nishati ya jua ambao utasaidia katika kutunza
mazingira na kupunguza gharama za uendeshaji ambazo zitatuwezasha kutoa huduma
kwa ufanisi Zaidi na kwa gharama nafuu ili kuwafikia watanzania wengi zaidi na
kusogeza huduma mbambali za kijamii karibu na wananchi zikiwemo huduma za
Elimu, Afya na Mawasiliano. Kazi kubwa kwa wananchi nikulinda huduma hizi na
kuzitumia vizuri kwa shughuli za maendeleo vijijini”.
Mawasiliano ndio chachu ya maendeleo
hivyo tunaamini kwa kutumia umeme wa jua hata gharama za uendeshaji zitapungua
hivyo kuwezesha ktoa huduma zenye viwango vya juu kwa gharama nafuu kwa
watumiaji na wateja wa Airtel nchini nzima aliongeza Mmbando”
Nawapongeza sana Airtel kwa ubunifu na jitihada hizi na vilevile nawaomba wafike Kijiji cha Mwauchumu,Tarafa ya Dutwa wilayani Bariadi,hasa kutokana na shughuli za kilimo na ufugaji wa ng'ombe na mbuzo.Katika kijiji cha Chumbi B hasa kitongoji cha Msomeni(Rufiji) ambako ni muhimu kwa shughuli za kilimo cha Mahindi na matunda na mbogamboga pia ni vizuri kuleta teknolojia hii.
ReplyDelete