Gari yenye nambari za usajili T 811 BQM likiwa limepinduka asubuhi ya leo maeneo ya Masaki kwenye barabara inayoelekea Salender,chanzo cha ajali hiyo hakikuweza fahamika mara moja na hakuna mtu aliyekufa,bali ni dereva ambaye alikuwa peke yake ndie ameumia kidogo.
Dereva wa Gari hiyo akiwa amekaa chini huku akiendelea kufanya mawasiliano ya hapa na pale kwa ndugu na jamaa.
Mashuhuda wakiangalia ajali hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kama huyo dereva wa hilo gari yuko mzima wa afya na anapiga simu kwa ndugu na jamaa zake, swali langu ni hili , inakuwaje wewe mwandishi wa habari hizi useme kwamba chanzo cha ajali hii hakikuweza kupatikana ?? shahidi si huyo dereva ?? kama ulipata nafasi ya kumpiga picha na picha zingine zote hizi,lakini ukashindwa kumuuliza kulikoni !!!!! something wrong with your report.kama hizi habari zimelenga kulielimisha Taifa,ni vyema kutupa sababu za ajali ili liwe somo kwa wengine,kama alilala wakati akiendesha au alikuwa akiongea na simu au ana sexting nakadhalika .Zebedayo msema kweli

    ReplyDelete
  2. Kweli nchi yetu nzuri na inapendeza..naona mandhari ya bahari kwa mbali..pole na ajali mhusika tushukuru Mungu umetoka salama salmini..

    ReplyDelete
  3. Vyuma chakavu sasa, ukimwuliza dereva atasema aliona jini.

    ReplyDelete
  4. Kujua chanzo cha ajali ni uchunguzi na si kila ntu anaweza. Ndege ikipata ajali huwa inaundwa tume ya wataalamu kuchunguza lakini gari dereva anaweza kuulizwa kuwa anadhani nini chanzo cha ajali. Aghalab madereva wa malori husingizia breki zimefeli wanapokusudia kuwaonea wenye vigari vidogo. Wataalamu wapo wa kila fani hivyo kila mmoja aachiwe afanye kazi yake.Kama unaumwa nenda kwa daktari na si kwa seremala.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...