Bw. Bayuni U. Sambilema alifika kutibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili siku kadhaa zilizopita. Akiwa mojawapo ya vyumba vya kutolea huduma alisahahu vitambulisho vyake muhimu sana.
Mojawapo ya kitambulisho cha kazi kinaonyesha kutolewa na Halmashauri ya Magu-Mwanza. Naomba yeyote anayemfahamu Bayuni U. Sambilema amwambie aje kuchukua vitambulisho vyake Ofisi ya Uhusiano, Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Pia anaweza kuwasiliana na Mimi kupitia 0755 64 86 36.



Tunashukuru kwa nia yako nzuri, lakini ungeweza kutoa taarifa bila kubandika kila kitu hewani. Watu hawaaminiki siku hizi. Identity theft ndugu yangu. Bongo kweli tambarare.
ReplyDeleteHuu sio ustaharabu!
ReplyDeleteHata kama ni kumsaidia sio vzr kuanika details zote hizo hadharani, heri kuandika jila lake ama kuficha details muhimu sababu wenye nia mbaya wanaoweza kutumia details hizo vibaya.
Uliyeweka IDs hizo ili muhusika akutafute umefanya jambo jema sana la kiungwana laki taf muombe Michuzi avitoe vitambulisho vyote haraka na uweke jina la muhusika tu kwani ni hatari mno (vinaweza kutumiwa vibaya na watu mtandaoni popote pale duniani katika Identity theft au hata fraud). PS.Michuzi vitoe hara mno taf - weka jina la muhusika tu au ziba details kama acc numbers n.k) thanks. Mdau wa IT Security.
ReplyDeleteAsante kwa nia yako njema lakini nadhani umefanya makosa kuanika kadi/vitambulisho vyote hasa vya benki.
ReplyDeleteUngetumia busara ya kupiga simu aidha kwa mwajiri wake au NHIF wakamtaarifu akaja kuvichukua kwako.
ReplyDeleteHongereni sana,
Hospital ya Muhimbili imekua faithful siku hizi yaani mtu kaacha vitambulisho alafu mmeamua kutangaza kabisaa Hongera sana mdau wa muhimbili kwa kuonyesha upendo wa ajabu hivyo na Mungu akubariki sana
Nakumbuka nili mpeleka baba yangu MOI kwenye physiotherapy tukaacha simu na begi lake mezani kufika kwenye gari ndo tunakumbuka kurudi kuulizia wakasema hawajaona chochote na wakati kalazwa hapo akiwa hoi akafariki tukarudi kufuata dawa zetu coz zilikua expensive sana wakasema zimeshatupwa
Ulichofanya si vizuri hata kidogo huu unafiki wa ambao watanzania wote unatusumbua,ustaraabu hakuna usipokuwa unafiki tu!
ReplyDeleteUwiii
ReplyDeleteAnkal Michu. Ondoa hivyo vitambulisho. kwa kuvianika hapo jamaa kishakwisha.
Uwiii
Ankal,
ReplyDeletenaona wadau wengi wamestukia ustaarabu wa msamalia mwema kuhusu kutangaza kupotelewa na vitambulisho, yaelekea kama kungekuwa na medicl journal yake wangeiweka hadharani. huu sio utaarabu. Hii nahesabu kama mara ya tatu, watu wanaokotoa vitambulisho au pasi ya kusafiria, wanaweka picha, majina na mwaka wa kuzaliwa. hawa wa mUhimbili, wamekweka vitu ambavyo ni habari binfsi za siri za mhusika, akaunti, kazi yake, cheo, nk..Nadhan Ankal, blogu yako kama vyombo vya habari vingine, lazima kufilter habari zinazoukuja, nadhani ndio kuhariri. Kama unakumbuka, kuan mtu aliwahi kutuma picha ya dada mmoja UK, kwamba anatafuta mchumba baada ikaonekana kanyabwoya. Haya , nyingine ilikuwa email ya kashafa ya mfanabiashara mmoja Marekani, LOs Angeles, baadae ikaonekana jama walikuwa wanataka kumharibia..kwa hiyo, ni vizuri, timu yako y aglobu kuwa makini ili watu wenye nia nzuri na mbaya wasikiuke haki ya ubinadamu ya kijisitir(privacy?). kama unavyotahadharisha watu wasichafue hewa wakati wa maoni, maoni mngine tupi kapuni, kwa sababu kama kikiandikwa hapa na ikanonekana ilikuwa majungu basi blogu hii ndio inawezeka kwajibishwa ama kisheria au kupoteza hadi..itunze hadhi ya blogu na watunzie wadau hadhi zao, hao wa Muhimbili ni kama wamevua mtu nguo..vitambulisho vyote unaweka hadharani, wakati mtoaji hajaweka hata jina, ila namba ya simu na ofisi anayofanyia kazi!
nawasilisha,
Omuburi
ReplyDeleteOVERREACTING
Madai yote ya hawa wenzetu 'security consious' to me does not hold water.
Hebu tupeni mifano michache VIPI "mtu mbaya" ataitumia hiyo COPY ya leseni hapo na "Identity theft" ina maana watu wawe wanaficha mpaka sura kwenye matangazo ya vifo si ndio?
Is this too much movies au too much novels?
If that's the case, then people should stop putting their photographs on lost passports, citizenship applications, death announcements, and much more scenarios where people post their photographs.
Tarehe ya kuzaliwa na picha, mtu aibiwe identity yake?
Sikatai, tupeni mifano. Mimi sidhani.
Ninachoshangaa huyo muhusika ni:
ReplyDelete1.Atakuwa anaendesha vipi gari wakati Leseni hana mkononi kwa sasa?
2.Atachukua vipi pesa Benki akiwa safarini nje ya eneo lake bila ATM card?
3.Atakuwa na uhakika gani atakapotakiwa ama kujitambulisha wakati ID kitambulisho chake kama cha kazi kwa sasa hana?
Pana maswali mengi ya kujiuliza kuliko majibu!
Hakuna fedheha kubwa kama kupotelewa na vitu kama:
ReplyDelete1.Kadi za Benki, haswa zikiwa zote ndani ktk mkebe kwa mkupuo!
2.Kupoteza Leseni ya gari, Vitambulisho vya kazi au vyovyote mfano Pasipoti!
3.Kupoteza simu!
Ohhh usiombe una changanyikiwa !
Mdau wa (9) Anonymous wa Tue Sep 25, 02:40:00 PM 2012
ReplyDelete......Sikatai, tupeni mifano. mimi sidhani.
Elewa Kiongozi ya kuwa ugumu wa maisha ni kipimo cha akili.
Zingatia ya kuwa Mamlaka kama TRA, MABENKI na IDARA NYETI zingine zinazotoa nyaraka mbalimbali zikiwa kazini huko Makao Makuu, vivyo hivyo (huko Msituni manyasini, kizani) WAZEE WA MTALIMBO WAPO BUSY HUKO VICHOCHORONI, MITAA YA KARIAKOO GEREZANI, MITAA YA JANGWANI KARIAKOO AMBAKO KUNA MITAMBO YA UCHAPAJI NA UFYATUAJI WA VITAMBULISHO!
KILA KITU CHINI YA JUA , KILA KITU KINAWEZEKANA AMINI USIAMINI !
HUWEZI KAUMINI MACHO YAKO VITU HIVI VINAFYATULIA MITAANI HUKO KARIAKOO GEREZANI NA JANGWANI.
1.KADI ZA BENKI (ATM)
2.LESENI ZA UDEREVA (HIZI MPYA ZA TRA ZA KADI)
3.KADI ZA KUPIGIA KURA
SASA HAPO KAMA MTU ANAPATA KADI YA BENKI YA MUHUSIKA NA NYARAKA KAMA PASIPOTI AMBAYO INAYO SAINI NDANI YAKE NI KUWA ANAFANYA HIVI:
(i)ANAFYATUA KADI YA KUPIGIA KURA
(ii)ANATAFUTA MTU WA KUFANANISHA NA MUHUSIKA ANAMPANGA ANAINGIA DIRISHANI KUCHUKUA PESA,
(iii)ANAKUWA AMEJIFUNZA KUPIGA SAINI HALISI YA MUHUSIKA AKITUMIA KADI YA KURA NA KUONYESHA KADI YA ATM DIRISHANI NDANI YA BENKI!!!
(iv)FWEDHA ZINATOKA DIRISHANI (sio kwenye ATM) KIULAINIII!!!
UPO HAPO?
Mdau wa Tisa Tue Sep 25, 02:40:00 PM 2012
ReplyDeletewewe OVERREACTING
Hujawahi kusikia pana namba zingine (watu) usipige sahihi akiwepo?
Akiona unavyopiga ama akipata sample ya sahihi yako looo umekalia kuti kavu!
Utakuta akaunti yako Benki nyeupee!
Wewe Mdau Tue Sep 25, 02:40:00 PM 2012
ReplyDeleteHizo nyaraka zote mpaka Leseni za kadi za sasa za Udereva za sasa vinafyatuliwa hukoo miferejini.
Hapo baada ya kufyatua ID hiyo Leseni ya Kadi inatafutwa Namba ya akaunti ya Benki na saini, halafu anatafutwa mtu wa kufananisha anajifunza kupiga sahihi halisi anazama ndani dirishani Benki akiwa na hiyo ID ya kufyatua mkononi.
Anafika dirishani ameshajaza fomu za kuchukua anaonyesha ID njanja lile, anahesabiwa FEDHA na Karani wa Benki, anapiga sahihi kama vile ni mwenyewe halisi!
pesa hiyooo inatoka!
Tue Sep 25, 02:40:00 PM 2012
ReplyDeleteMbona kazi ndogo sana!
Wewe Bandugu,
1.Inachongwa Mtaani huko Mifenesini Leseni hiyo ya gari
kwa details hizo.
2.Ni mfanyakazi wa Halmashauri
(Serikali za Mitaa) lazima atakuwa na Akaunti ktk Benki ya NMB inatafutwa Namba ya akaunti na saini.
3.Anatafutwa Dingi Msanii, Mukulima wa Mujini anayefanana naye au hata 'Mwigizaji' Kijana yeyote atakaye weza kupindisha sura akafanana naye anapatiwa ID ya kujifunza kupiga saini hiyo.
4.Anazama na Leseni ya gari ID ya kufyatua Mtaani anajaza fomu kwa namba ya Akaunti iliyopatikana na kupakuwa Fedha na kupiga saini kupitia Dirishani ndani !!!
Huku watu wanasikilizia nje, mara Dingi anatoka nje ya Benki na mfuko wa kaki jasho limezagaa upara mzima kichwani anahema kama chura!
5.Watu wanakaa mkao wa kula panga linapita mgawo!
Huyo Babu wa Halmashauri ya Magu anacheza wa watu ya mujini?
ReplyDeleteEnhee wazee wa Mabao ya Mujini hapo wala hawahangaiki na Benki kama Barclays, Stanbic na CRDB wao wanacheza na NMB ambayo wanajua ipo hadi Magu!
Atakapo kuja tembelea NMB Tawi la huko Magu atakuta akaunti yake ya Benki inacheka!
Wewe Namba 9 Mtoa maoni,
ReplyDeleteKwa umri aliofikia huyo babu ktk kazi huko Halmashauri Magu wazee wa mnemba Bongo Daslam wanajua lazima atakuwa na akiba ya kutosha!
Wana copy na ku paste details hizomkwa kufyatua Mtaani, anazama mstari wa mbele kamanda Dingi mwingine wa Mujini.
Wanazama mtamboni wanakomba zooote NMB sio pengine!
Huyu babu wa Magu Bayumi Sambilenga Usanga nacheza na wazee wa Bilinanaz ,Azzam take away Bongo Daslaam?
ReplyDeleteWatakomba mafao yote ya kazi yake Halmashauri ya Wilaya Magu, na akiba nyingine!
Atakuta akaunti yake ya NMB ina 'zero balance' huko Magu Branch!
Wewe Namba 9 pana sehemu moja inaitwa Azzam take away jijini Darisalama.
ReplyDeleteAtatafutwa pale maskani Dingi mujanja mujanja anayefanana hata kidogo na huyo babu hapo halafu wasanii watazama mgodini watatoa vitu vyote 'geniune copy zake' atakabidhiwa Jembe wa Azzam atazama mtaa ule ule NMB ya Mako Makuu Mtaa wa Jamhuri atatoka nazo tu!
Watu wapo Azzam wanasubiri babu arudi kutoka Benki huku wakinywa juisi za Boksi za Azzam za embe!
Tue Sep 25, 02:40:00 PM 2012
ReplyDeleteMdau kama hufahamu waulize Maafisa wa Usalama na Polisi wakwambie!
Kulingana na mwamko wa uwezo wa kiusanii unaotokana na ugumu wa maisha hakuna kitu chini ya jua inashindikana!
Ile kwanza kupoteza kwake hivyo vitu vingeangukia kwa watu wa sanaa ohhh angekwisha lia machozi huyo babu!
Huwezi amini waweza kumvutia hadi akiba yake ya mafao ya uzeeni ktk Mifuko ya Akiba ya PPF au LAPF kama za kwao vile!
Kwa Wasanii wa Mujini hakishindikani kitu!
ReplyDelete1.Anatafutwa mtu mwenye likipara kama huyo babu wa Magu,
2.Au hata kama hana kipara anavyoa nywele zoote na kuwa hivyo hviyo!
3.Hata kama hawafanani anavimbisha mashavu na kushusha uso ili mradi kipindi akiwa Dirisha la Benki afanane na babu!...hadi anavuta pesa !,,,mchezo Jijini Kisomo watu wanjua maigizo balaa!
Yeye babu yuko Magu huko Kwimba kwake, mwanawane watu wanavuta pesa yote Mujini Darisalama!
Ohhhh,
ReplyDeleteAnacheza na Majembe ya Azzam take away na Bilicanas?
Huyo Mzee atakaa zake Magu akiendelea na kuchapa kazi Halmashauri ya Wilaya huku Bongo Daslaam Wasanii wakiwa wamesha komba mafao yake ya uzeeni LAPF na PPF zamaniii!