Balozi Tuvako Manongi akimkabidhi Katibu Mkuu Ban Ki Moon hati zake za utambulisho katika hafla iliyofanyika siku ya jumatano ofisini kwa Katibu Mkuu hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Balozi Manongi alikuwa kati ya Mabalozi sita waliowasilisha hati zao siku hiyo ya jumatano, ikiwa ni siku chache kabla ya Kuanza kwa Majadiliano ya Mkutano wa 67 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, mkutano utakaohutubiwa na viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa
Katibu Mkuu akiwa na Balozi Manongi mara baada ya kukabidhi hati zake.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akiwa katika mazungumzo mafupi na Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Tuvako Manongi mara baada ya kuwasilisha hati zake. katika mazungumzo hayo Katibu Mkuu alielezea matumaini yake ya kuendelea kufanya kazi kwa karibu na Balozi huyo pamoja na Viongozi wakuu wa Tanzania. Kwa upande wake Balozi Manongi aliwasilisha salamu za Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete alizotumwa kwa Katibu Mkuu, na pia akaahidi kutumia uwezo wake wote kutetea maslahi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, pamoja na kushirikiana na Katibu Mkuu katika shughuli za kila siku za Umoja wa Mataifa.
Na
Mwandishi Maalum
Katibu Mkuu akiwa na Balozi Manongi mara baada ya kukabidhi hati zake.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akiwa katika mazungumzo mafupi na Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Tuvako Manongi mara baada ya kuwasilisha hati zake. katika mazungumzo hayo Katibu Mkuu alielezea matumaini yake ya kuendelea kufanya kazi kwa karibu na Balozi huyo pamoja na Viongozi wakuu wa Tanzania. Kwa upande wake Balozi Manongi aliwasilisha salamu za Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete alizotumwa kwa Katibu Mkuu, na pia akaahidi kutumia uwezo wake wote kutetea maslahi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, pamoja na kushirikiana na Katibu Mkuu katika shughuli za kila siku za Umoja wa Mataifa.
| Balozi Tuvako Manongi, akiwa katika picha ya pamoja na maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi mara baada ya kuwasilisha hati za Utambulisho kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. |
Balozi
wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Tuvako N. Manongi jana Jumatano amewasilisha hati
zake za utambulisho kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon.
Balozi
Manongi alikuwa kati ya Mabalozi Sita
waliowasilisha hati zao siku hiyo ya jumatano ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 67 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
utakaowahusisha Wakuu wa Nchi na Serikali
kutoka nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa.
Hafla
ya kukabidhi hati hizo imefanyika Ofisini kwa Katibu Mkuu na kushuhudiwa
na baadhi ya Maafisa Waandamizi kutoka
Ubalozini .
Baada
ya kukabidhi hati hizo, Katibu Mkuu Ban Ki Moon alifanya mazungumzo na Balozi
Tuvako Manongi.
Katika
mazungumzo hayo, Katibu Mkuu amesema
anaendelea kuitegemea Tanzania
kama nchi kiongozi na mshawishi
katika kusukuma mbele ajenda zake, zikiwamo zile zinazolenga kufanya mapitio ya baadhi ya majukumu ya Umoja wa Mataifa.
Akasem.“Ninayo
mahusiano ya karibu na
ushirikiano mzuri sana na Rais
Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Mambo ya Nje
Bernard Membe na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wangu
Asha-Rose Migiro. Mimi na wewe tunafahamiana vizuri tumefanya kazi kwa karibu. Ninakutumainia wewe na nchi yako kwamba mtaendelea kuwa msaada
kwangu na kushirikiana nami kwa karibu”
akasititiza Ban Ki Moon.
Aidha
Katibu Mkuu huyo wa UM , ambaye alionyesha wazi kufurahishwa na Uteuzi wa Balozi Manongi kuwa Balozi
katika Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika UM, na hasa ikizingatiwa kwamba alikuwa mmoja
wa maafisa wake waandamizi kabla ya uteuzi huo. Na amemhakikishia Balozi ushirikiano wa karibu na kwamba milango iko wazi wakati wowote
akimhitaji.
Kwa upande wake, Balozi Manongi pamoja, na kufikisha
kwa Katibu Mkuu Salamu rasmi alizotumwa na Mhe. Rais Jakaya Kikwete amesema, atatumia uzoefu wake kusukuma mbele
ajenda si tu za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa bali pia hasa zile ambazo zina maslahi kwa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Afrika kwa Ujumla.
Sehemu ya
salamu rasmi za Mhe. Rais Jakaya Kikwete kwa Ban Ki Moon, zilikuwa ni pamoja na kumshukuru Mkuu
huyo wa UM kwa uamuzi wake wa kuitisha mkutano maalum utakaojadili mgogoro na
kuzotora kwa usalama na amani
katika eneo la Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( DRC).
Mkutano huo utawashirikisha
viongozi mbali mbali wakiwamo wakuu wa Nchi na Serikali na wadau wengine kujadiliana ambapo watajadiliana na kubadilishana mawazo
kuhusu namna bora ya kuchagia
upatikanaji wa amani ya kudumu katika eneo la Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mkutano huo
utafanyika Septemba 27 hapa Umoja wa Mataifa na unatarajiwa kutoka na
tamko rasmi.
Ikumbukwe pia kwamba,
Rais Jakaya Kikwete ni Mwenyekiti wa Asasi ya
Siasa, Ulinzi na
Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo
ya Nchi za Kusini mwa Afrika ( SADC) na amekuwa mstari wa
mbele katika kutafuta suluhu na amani ya
kudumu katika eneo hilo na Mashiriki ya
DRC.
Balozi Tuvako Manongi anakuwa Balozi wa
kumi na Nne (14) tangu kuanzishwa
rasmi kwa Ubalozi wa Kudumu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika Umoja
wa Mataifa.
Mabalozi wengine ambao wamewahi kushika wadhifa huo huko nyuma, ni Balozi Vedast K. Kyruzi, Balozi A.Z. Nsilo
Swai, Balozi Chifu Erasto A.M. Mang’enya, Balozi John W.S. Malecela, Balozi Akil
B.C. Daniel, Balozi Salim Ahmed Salim, Balozi Paul M. Rupia, Balozi Mohamed Ali
Foum, Balozi Dr.Wilbert K. Chagula,
Balozi Anthony B. Nyaki, Balozi Daudi N. Mwakawago, Balozi Dr.Augustine P.
Mahiga, na Balozi Ombeni Y. Sefue.
Balozi
Manongi atafanya kazi kwa karibu na kwa ushirikiano mkubwa na Naibu Balozi Ramadhan Muombwa
Mwinyi anayetarajiwa kuwasili kituoni wakati wowote.




Huyo Afisa mdogo dogo huko mwanzo wa picha kushoto anaitwa nani na yukp idara gani?
ReplyDeleteHuyo ofisa anaitwa Dogo Janja yupo idara ya mawasilaino.
ReplyDelete