Sehemu ya uharibifu uliofanywa na wavamizi hao huko Ugiriki usiku wa kuamkia leo
Habari ankal Asante kwa kuniwekea habari zangu nyingi kuhusu Ugiriki, licha ya baadhi ya watu kuona tunawabania kuja Ugiriki na kuuliza kwa nini nyie mpo kama kuna matatizo Ukweli ni huu Chama cha XRISI AVGI au Golden down(Neo Nazi) kimeanza piga piga ya wageni wakiongozwa na wabunge wao ambao polisi inashindwa kuingilia kati wakiwepo.
Yaani usiku wa kuamkia leo Septemba 26, 2012 ofisi za Jumuiya ya watanzania ziliharibiwa vibaya na baadhi ya watu kujeruhiwa. Licha ya kuwepo kwa Polisi bado walishindwa kuzuia tukio hilo na kuonekana polisi wakiwapa mgongo kabisa Watanzania baada ya hapo walielekea maeneo mengine ya mabaa ya wageni yaliyopo karibu na kuharibiwa vibaya pia Baadhi tu ya picha na news pia zipo kwenye mitandao mingi tu.
Mdau Umangani
Wadau wkiwa nje ya ofisi za Jumuiya iliyovamiwa






Huku si mnaona tunavyochinjwa na vyombo vya Uhasama! Kazeni boot, maisha ni mapambano!
ReplyDeletepoleni sana wadau ila rudini kwenu jamani.
ReplyDeletehata huku maisha yapo.
yaani hawa watu millioni 41 hawatoshi kuonesha kua maisha yapo?
or what else do you want?
Kufeni kidume lakini bongo msirudi mpaka mpate pasi ya kigiriki halafu mtahamia UK.
ReplyDeleteUgiriki, Portugal, Italy, Spain, na baadhi ya nchi nyingi za Ulaya uchumi uko kwenye matatizo makubwa sana.
ReplyDeleteNyie wenye mabaa na biashara zingine kwenye nchi hizo lazima mtakuwa mnaonekana mko na 'hali nzuri'.
Hivyo basi ni lazima watakunyimeni amani maana kibao kimegeuka, cha msingi wekezeni zaidi nyumbani maana sisi huku thamani yetu huwa ni ileile, IKO JUU.
Msikubali kuonewa Mnaweza kuwashitaki kwenye mahakama za kimataifa.
ReplyDeleteMimi nilisha washitaki wangu na nikishinda kesi watanilipa zaidi ya dola 19000.
Inaudhu sana ninapoona Watanzania wananyanyaswa.
We subiri tutengeneze nyumbani ili turudi na wao wakija kule na ujinga wao wa unaziz tuwape kipigo kitakatifu.
Poleni sana wenzetu wa Ugiriki, wakati umefika na sisi kuwafanyia hivyo kwa wagiriki waliopo hapa nchini ili nao waone MUZIKI wetu.
ReplyDeleteKaka mkiona hivyo hamtakiwi tena la msingi kama si cha sekondari mwaanzage kufungasha!!
ReplyDeleteNa huku baado ardhi kubwa ujuzi mlonao toka huko majuu tukiuchanganya na ushamba wetu tutavuka!
MABO YA KUMCHUKIA MGENI SIKU HIZI YAPO KATIKA MATAIFA MBALIMBALI KAMA AFRICA KUSINI, KENYA, UK, HATA TANZANIA YAPO. POLENI KWA USUMBUFU.
ReplyDeleteMATATIZO YA KIUCHUMI NA KIJAMII YANAPOTOKEA SEHEMU YOYOTE WAGENI HUBEBESHWA LAWAMA HATA KAMA HAWAHUSIKI
Piga, ua, galagaza, SIONDOKI, tutabanana hivi, hivi, inajaa ndoo ya maji siyo NCHI.
ReplyDeleteSasa nyie mko nchi za watu bendera za nini? Nitafurahi sana siku nikisikia vibaraka wa CHADEMA au CCM wakipingwa mkong'oto na uwe wa nguvu. Kama na uchungu na nchi si mrudi? Hata hapa nchini si tunawalaumu wachina, wahindi wa wazungukwenye madini? Mbao yaho yako dunia nzima, hata ukisema ni kwa sababu ni weuzi mbona Afrika ya kusini mambo yale yale?
ReplyDeletemimi watu wanaosihi walio nje kurudi bongo nawashangaa. MBONA wao wameng`ang`ania DAR, warudi jijini waliokotokea KAMA KWELI WAO WAZALENDO . Mmewaacha ngugu zenu hawana maji safi, mnapoteza muda online kuwasiliana na walio ugiriki !!
ReplyDeleteNinajiuliza Kwanini walivamiwa watanzania tu? Mliwakosea nini? au hapa Tanzania tumefanya nini kuwakasirisha huko kwao?
ReplyDeleteSasa mtalijua jiji bora mie niko tz napata ugali wangu na dagaa kuliko kipigo!
ReplyDeleteWaliovamiwa siyo watanzania tu bali hata watu wa mataifa mengine.
ReplyDeleteMdau wa ugiriki