Chama Cha Mapinduzi ,Tawi la  Uingereza Jana Tarehe 09.09.12 kimefungua shina Jipya katika Mji wa Leicester kwa changamoto ya hali ya juu, hoja nzito na kishindo kikubwa.
Katika ufunguzi huo uliosimamiwa na Katibu Mpya wa Tawi Bi. Mariam Mungula (pichani juu kulia) alisisitiza suala la umoja kwa wana CCM na wanadiaspora kwa ujumla katika kutoa mchango wao kwa sauti moja ili kuweza kuwa na Nguvu ya pamoja na kuchangia katika  kuboresha ufanisi wa Serikali ya Tanzania kwenye Nyanja mbali mbali za huduma za kijamii na maendeleo ya kiuchumi kwa faida ya watanzania wote. 
 Katibu Mpya wa Tawi Bi. Mariam Mungula akigawa kadi kwa wanachama wapya
 Katibu Mpya wa Tawi Bi. Mariam Mungula akigawa kadi
Katibu Mpya wa Tawi Bi. Mariam Mungula akitoa kadi kwa furaha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Ndugu zangu ,hizo kadi za uanachama ningependekeza ziwe na saizi ndogo kama ile ya drivers license, zi fiti kwenye wallet.Au nimekosea ??? maoni tu ,ila nitashukuru kama mutaniunga mkono .Zebedayo msema kweli

    ReplyDelete
  2. UTANZANZIA AU UCCM NA UCHADEMA..NI PALE MAREKANI ITAKAPOFUNGUA MATAWI NCHI ZOTE DUNIA..MARA DEMOCRATIC AU REPUBLICAN,
    HATUNA UKABILA LAKINI TUNA UCHAMA..IT HAS BEEN CANCER THAT IS SILENTLY KILLING OUR NATIONAL UNITY GUYS, LETS GET RID OF IT GUYS

    ReplyDelete


  3. Mdau wa pili yaani wewe nyamaza kimya tulifundishwa tukiwa bongo uki muamsha alie lala utalala wewe yaani mimi kila mara nikifungua hii blog kuangalia any good news about tanzania sioni cha maana kwa kweli alafu wanasema rudini tanzania mjenge nchi hahaha yaani Mungu anisaidie ila nitarudi tu kuzikwa kijijini kwetu machame lakini sio kuishi kwa ujinga huu wa watanzania

    ReplyDelete
  4. piganieni kwanza haki yenu ya Uraia wa Nchi Mbili,kisha kikatiba muwe na haki ya kushiriki uchaguzi mkuu hata mkiwa Uingereza au Marekani au popote pale nchi za nje!Msidanganyike kirahisi hivyo,kuwa na kadi ya chama na wewe uko nje ya nchi,pengine una uraia wa huko,kadi itakusaidia nini?Na hii biashara ya kufungua matawi ya vyama vya siasa nje ya nchi imetoka wapi na nini agenda au kusudio lake?iwapo hapa hapa nyumbani ndani ya nchi mambo yanatushinda?sio watanzania wote nchini wenye kadi au ufuasi wa vyama vya siasa!Dont be Fooled!

    ReplyDelete
  5. Hii kitu inaitwa U-politic ilianzishwa na Mhe. Nannihii kule nanihii. Wanadiaspora wakampiga maneno mingi. Alipohamishwa na Bw. Mkubwa kuhamia nanihii nako akapanda mbegu za Usiasa ambazo sasa zimeshamiri.
    Hapo awali Wanadiaspora wa Tanzania walikuwa wako bize na kubeba maboxi na kutuma hela nyumbani kwa ndugu zao. sasa wanatumia muda mwingi kuhangaika na siasa.
    Tunashangaa sana kwa nini huu ugonjwa wa siasa ulizikumba zaidi nchi mbili hauambukizi diaspora walio katika nchi nyingine kama Rwanda, Burundi, Angola, Sudan, Kenya, Uganda, jamani, China wala Oman.

    Mwenye chanjo atupatie tafadhali

    Mzee wa Migomigo

    ReplyDelete
  6. CHADEMA hawana spporters nje ya nchi, pamoja na kujitosa kwao, kwa sababu wanachoona watu wengi kwenye TV ni maandamano na vifo katika campaign zao sasa kidogo kuna kawoga. Kama wanaona wanapata umaarufu, na kujiharibia vile vile kuko. Watanzania waoga wakiona mambo yenyewe ndio kwenda kufa wanarudi nyuma. Nyie endeleeni, 2015 msije mkasema ooh tumeibiwa kura.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...