Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU, yenye maskani yake kule ujerumani, inayokamatia taji la kimataifa la "IDA-International Diaspora Award' inatarajiwa kutumbuiza katika onyesho lingine makubwa  leo jumamosi ya 15.9.2012 
Kikosi kazi hicho kitapeleka nguvu zote katika maonyesho makubwa ya biashara ya kiafrika "AFRIKA-MESSE" Bremen,yatakayafanyika mjini Bremen,Ujerumani.
Bendi hiyo inayotamba CD mpya "Bongo Tambarare" ambayo imeshatua kwa kishindo katika vituo vya redio mbali mbali ndani na nje. Ngoma Africa band iliyoanzishwa mwaka 1993 muhasisi wake Kamanda Ras Makunja,  wa FFU,ambaye pia ndiye kiongozi wa kikosi kazi hiko. Kikosi kazi hiko kilichojizolea washabiki kila kona duniani kimekua tishio la  kimataifa,inasemekana kuwa ndio bendi pekee ya kiafrika iliyo fanikiwa kuteka nyoyo za washabiki wa kimataifa na kuwafanya washabiki kuwa ndio wamiliki wa bendi hiyo.
Usikose kuwasikiliza bofya at www.ngoma-africa.com 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...