Baadhi ya Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya habari wakisililiza hotuba ya ufunguzi wa semina ya siku mbili iliyoandaliwa na Idara ya Uhamiaji Makao makuu na kufanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Edema, mjini Morogoro.
Baadhi ya Wahariri wa Vyombo vya habari akiwemo wa Gazeti la Habarileo, Joseph Kulangwa ( wapili kutoka kushoto) pamoja na Jesse Kwayu wa Gazeti la Nipashe , wakisoma moja ya habari iliyokuwemo kwenye mtandano wa Intaneti kupitia kompyuta ya mkononi, kutoka kwa mmoja wa wahariri wanaoshiriki semina hiyo , Septemba 15, mwaka huu.
Kwa mujibu wa Uongozi wa Idara hiyo ,katika semina hiyo, mada mbalimbali zilitolewa na Maofisa wa Idara ya Uhamiaji , ambazo ni pamoja na Sheria zinazosimamia shughuli za Uhamiaji Tanzania, Sheria ya Uraia wa Tanzania ya mwaka 1995, Huduma ya Vibali vya Ukaazi na Pasi kwa wageni sambamba na suala la udhibiti wa Wahamiaji haramu nchini.
Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maofisa wa Idara la Uhamiaji nchini , mara baada ya kufunguliwa kwa semina Septemba 15, mwaka huu, na Kamishina Mkuu wa Idara hiyo, Mwichumu Hassan Salim kutoka Zanzibar na kufanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Edema, mjini Morogoro.Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii,Morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...