Mvutano kwa wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kata ya Kichangani mjini Morogoro wakigombea kuzika maiti ya mtoto mdogo wa miezi saba baada ya familia kugawanyika katika itikadi za kisiasa.
Home
Unlabelled
Siasa yaingia mazikoni morogoro
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Mungu atunusuru na mambo kama hayo kama jamaa anavyosema tunapoenda maziko yatakuwa biashara si moyo wa watu kwenda mazikoni kwa nia nzuri Allah atuepushe na haya.
ReplyDeleteJENGINE CCM WALIOENDA KWA NIA YA KUONA WENZAO CHADEMA WAMESAIDIA HAWAONI AIBU? NA CHADEMA PIA KAMA KUSAIDIA MNGESAIDIA NA KUKAPEMBENI AU KUTEKELEZA BILA BENDERA AU KUTANGAZIA ILA KUSAIDIA KWA NIA YA MAONYESHO NAYO HAIFAI VYAMA WACHENI KUVURUGA WATU LEO TU MASIKINI MTOTO TU HUYO ALLAH ANAMCHUKUA MAHALA PEMA JE INGEKUWA MTU MZIMA MNGEUWANA KWA CANCeR YA SIASA TUBADILIKE WA-TANZANIA.
duh hii sasa hatari watanzania tunapoelekea sio kuzuri mambo ya siasa mpaka mazikoni hivi kweli kwa mungu kuna vyama?
ReplyDeleteHaya sio makubwa ndugu zangu kwani huku Zanzibar yalitokea na inashangaza kwamba mlio wengi Mrima hamkujua au mlifunga macho na masikio mkiona ni ya Wazenji tu? Hakuna budi kwetu tuamke na kuvisusa vyama au wanasiasa wanaoleta mtafaruku wa jamii kwa faida zao. Tujifunze kwa wenzetu wale walio ona "Arab Spring" ndio njia njema ya kupata madaraka tu waangalie kwa makini kwani Afrika hakuna "Spring" bali ni Masika au Vuli nazo bila kipimo huleta hasara zaidi kuliko mafanikio. Napenda Kutoa mkono wa pole kwa wafiwa na kuwaomba wawe wavumulivu katika kipindi hiki kigumu kwao. Umoja wa Watanzania ndio sifa pekee tuliyo nayo shime tuilinde.
ReplyDelete