Habari na picha na Mindi Kasiga
Mkutano wa 520 wa Kamati ya Kimataifa ya Ushauri Kuhusu Pamba (International Cotton Advisory Committee) umefanyika Ubalozi wa Tanzania Washington DC tarehe 20 Septemba, 2012, ambapo Tanzania ni Mwenyekiti kwa mwaka 2011/2012. 

 Mwakilishi wa Tanzania kwenye Kamati hiyo ni Mkuu wa Utawala na Fedha Bibi Lily Letawo Munanka ambaye sasa ndio Mwenyekiti baada ya kuwa Makamu wa Kwanza wa Mwenyekiti 2010/2011 na Makamu wa Pili wa Mwenyekiti 2009/2010. ICAC ilianzishwa mwaka 1939 mjini Washington, DC kwa lengo la kusaidia nchi wanachama kuendeleza zao la pamba na kulipa nafasi katika uchumi wa dunia kwa ujumla.

Aidha Kamati hiyo hutoa taarifa mbalimbali za uzalishaji, biashara na matumizi ya zao la pamba na mabadiliko ya soko duniani ambayo yanaweza kusababishwa na mambo hayo matatu. Tanzania (Tanganyika) ilijiunga mwaka 1962 na ni miongoni mwa nchi wanachama 41. ICAC pia ni jukwaa la nchi wanachama kuzungumzia masuala mbalimbali ya kimataifa kuhusu pamba ambapo Tanzania pamoja na nchi nyingine zinazoendelea hutetea maslahi yao.
 Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico, Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar (aliyesimama), akiwakaribisha wajumbe wa Mkutano huo Tanzania House kabla ya mkutano kuanza. Waliokaa pembeni mwake ni Mwenyekiti wa Kamati, Bibi
Lily Letawo Munanka na Mkurugenzi Mtendaji Bw. Terry Townsend.
 Wajumbe waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar.
 Mwenyekiti, Bibi Lily L. Munanka akiendesha mkutano huo na wajumbe wakifuatilia. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa ICAC, Bw. Terry Townsend.
Mtakwimu wa ICAC, Bw. Andrei Guitchounts,  akitoa mlinganisho wa matumizi ya pamba kwa miaka 2 iliyopita (2010/11, 2011/12) na matarajio kwa mwaka 2012/13 na wajumbe wakifuatilia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...