Picture
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari walioathirika na mgomo Dkt. Paul Swakala (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam (picha na MoDewji blog)
Na MoDewjiBlog, Dar es Salaam -- Wanaodaiwa kuwa ni Madaktari wanaofanyakazi chini ya usimamizi wa madakatari bingwa (Intern Doctors), wamemwangukia Rais Jakaya Kikwete huku wakimwomba radhi kwa ushiriki wao katika mgomo wa madaktari uliosababisha maafa kwa baadhi ya wagonjwa.

Kwa upande mwingine wamekijua juu Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT) kuwa kimewasaliti katika kutatua matatizo yao kwa sasa.

Hata hivyo, wameomba radhi kwa Wananchi walioathirika na mgomo huo kwa usumbufu uliyosababishwa na mgomo huo.

Hadi sasa Madaktari 364, wako mtaani baada ya kusimamishwa kazi kutokana na kushiriki katika mgomo ambao umeisha hivi karibuni, baada ya kushawishiwa na wenzao wakiwemo viongozi wa MAT.

Akitoa tamko kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari hao, Paul Swakala alisema “Tulikaa na MAT kuzungumza juu ya kutusaidia kutatua kero zetu lakini wameshindwa kutusikiliza na baadala yake tumeamua kufika hapa na kutoa kilio chetu”

Kutokana na kusalitiwa huko, alitoa onyo kwa Madaktari wengine kuwa wanaweza kupima kama wataendelea kujiunga na MAT au la. Alienda mbali zaidi na kusema, hawako tayari tena kushiriki kwa namna yoyote katika migomo inayoweka rehani maisha ya Watanzania. Alisema, kwa hakika wanajutia kosa lao la kushiriki mgomo na wako tayari kurejea kazini ili kuendelea na kazi ya kuwahudumia Wananchi kwa moyo mweupe.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mwee, acheni usanii ninyi. Mlipie madhara/athari ya mgomo wenu kwanza ndio mtuombe msamaha.

    ReplyDelete
  2. Akili ya Ulimboka, changanya na yako!

    ReplyDelete
  3. Yote atalipa Mungu kwa ubaya wa maafa ua vifo vya wagonjwa mliyosababisha ingawa kifi hupangwa na yeye Mungu!.

    Yeye ndugu yetu Raisi wetu Mhe.Kikwete hana kinyongo na ninyi atawasamehe kama sisi wananchi tunavyo wasamehe isipokuwa mjifunze kuwa na busara zaidi kuliko jazba kama mnavyoona yaliyowatokea!

    ReplyDelete
  4. Raisi wetu Mhe.Kikwete,

    Punguza huruma zako ndugu yetu, hawa jamaa sio wa kuwasamehe kirahisi rahisi kama wanavyo tegemea!

    Hatuwezi kuwaamini kwa haraka haraka kwa mwenendo walioufanya!

    Angalia dharau kubwa kabisa waliyokuletea wewe mwenyewe Muungwana Raisi wetu kipindi kile,

    Angalia jinsi walivyoutesa umma wa wa Tanzania hadi kupelekea wimbi la vifo va wagonjwa kwa mgomo wao,

    Angalau ungewapa muda wa miezi mitatu (3) wafanyiwe uangalizi kabla ya kusamehewa kama watakuwa wamejirekebisha mwenendo wao.

    1.Kwa kuwa Udakitari ni kazi nyeti na inayofuata Maadili Kanuni na vigezo,

    2.Kuwa Dakitari kigezo sio kuwa na akili za kufaulu masomo ya Udakitari pekee badala ya kuwa na mwenendo, mwema, kujituma na kujitoa kuokoa, kujali na moyo wa Ulei,

    3.Udakitari hautunukiwi kama njugu panatakiwa na sifa za ziada pia,

    Mhe. Raisi tafadhali zingatia hayo mambo No.1, No.2 na No.3 kabla hujawasamehe hao Madakitari!

    ReplyDelete
  5. Kitendo mlichokifanya hakitegemewi kufanywa na mtu mwenye Taaluma inayotumia akili kama Udakitari!

    Hata Machinga wasiosoma hawezi kufanya ujinga kama mlioufanya ninyi Wasomi !

    ReplyDelete
  6. Wachekeni hahaha !

    Wazomeeni ooooooo!

    Uso umweumbiwa haya!

    Hapo ktk video ya You Tube huyo dada mwenye Blauzi nyeusi anajisikia aibu kubwa sana!

    ReplyDelete
  7. Madakitari ovyoooo!

    Angalieni ndio maana wahenga walisema 'USIMTUKANE MKUNGA WAKATI UZAZI UNGALI UNAO'

    Sasa wajameni nyie Wasomi Madakitari vile mlivyomdharau Raisi kipindi kile mkapandisha kiburi chenu, mnafikiri kama sio ninyi ni Raia wa nchi gani atakuja mjengea heshima Raisi wenu hapa Tanzania?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...