Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akipokelewa katika uwanja wa ndege wa Zanzibar wakati akirejea kutoka nchini Marekani na Uingereza kwa ziara ya wiki mbili.(Picha, Salmin Said-Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar
---
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amerejea nchini baada ya kumaliza ziara yake ya wiki mbili nchini Marekani na Uingereza.
Maalim Seif aliondoka nchini tarehe mosi mwezi huu kwa ajili ya kuhudhururia mkutano wa kimataifa unaohusiana na masuala ya demokrasia duniani, ulioandaliwa na taasisi ya National Democratic Institute katika mji wa North Carolina nchini Marekani.
Baada ya kumaliza mkutano na makongamano yaliyoandaliwa na taasisi hiyo, Makamu wa Kwanza wa Rais aliendelea na ziara yake katika miji ya Washington na London ambako alikutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa nchi hizo, pamoja na viongozi wa wa taasisi zinazoshughulikia sera za mahusiano ya kimataifa.
Akiwa mjini Washington, Maalim Seif alikutana na msaidizi Waziri wa mambo ya nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika Bwana John Carlson katika jengo la Wizara hiyo mjini Washington, kuzungumzia juu hali ya maendeleo ya siasa na demokrasia Zanzibar.
Pia alikutana na uongozi wa shirika la misaada la Marekani USAID, pamoja na kuzungumza na viongozi wa jumuiya ya wazanzibari wanaoishi nchini Marekani.
Huko Uingereza Maalim Seif alikutana na mabalozi wa nchi za Afrika pamoja na maveterani wa Uingereza, ambao walikutana kuzungumzia masuala mbali mbali yanayohusu maendeleo ya Zanzibar tangu kuundwa kwa serikali ya Umoja wa kitaifa.
Na
Hassan Hamad
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar


Kelele zote za HAKI SAWA KWA WOTE Kwishiney!
ReplyDeletemnyalu nakuunga mkona kwa maneno yako mwanangu haki sawa kwa sote kwishiney, ndo siasa hiyo ndo maana wanasema politics is a dirty games,ukizibwa mdomo ukapewa unachotaka na yako na familia yako yakakuendeeni basi unapoa kama maji ya mtungini, PENYE UZIA PENYEZA RUPIA JAPO KUWA SIWOTE WAKO HIVYO WENGINEWE NI WAKOMBOZI WA KIKWELI KWELI WA WANYONGE MFANO MZEE WA IKELAA MUNGU AMJALIYE KILA LA KHERI NA BARKA TELE AMIN.
ReplyDeleteSALAAM KUTOKA KWENYE NCHI YA BABA OBAMA(U.S.A)
ReplyDeleteWhat are you trying to say?