Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Viongozi pamoja na Vijana wanaoishi katika Nyumba za kurekebisha Tabia kwa watu waliokuwa wakitumia dawa za kulevya { Sober House } hapo Nyarugusu Wilaya ya Magharibi.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Baskeli Kijana Mlemavu Badri Ameir Issa ambayo itamsaidia katika harakati zake za Kimaisha. Msaada huo amekabidhiwa hapo Nyumba ya kurekebishia Tabia iliyopo Nyarugusu Shehia ya Pangawe Wilaya ya Magharibi. Kulia yao ni Mlezi Mkuu wa Nyumba hizo Bibi Fatma Sukwa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi  vyakula Mshauri Mkuu wa Nyumba saba za kurekebishia Tabia Unguja na Pemba  Bibi Fatma Sukwa  kwa ajili ya kusaidia Vijana wa nyumba hizo.     Wam,wanzo kulia yao ni mlezi wa Nyumba ya kurekebishia watu waliotumia dawa za kulevya ya  Mtaa wa Nyarugusu Shehia ya Pangawe Bwana Badru Nassor Ali. 

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kuwasaidia Vijana waliotengemaa baada ya kuacha matumizi ya dawa za kulevya kwa kuwapatia mtaji endapo vijana hao wataamaua kubuni na hatimae kuanzisha miradi ya kujiimarisha Kiuchumi.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akizungumza na Viongozi na baadhi ya Vijana waliomo ndani ya nyumba saba za kurekebishia tabia Unguja kwa watu waliokuwa  wakitumia  dawa za kulevya hapo katika moja ya nyumba hizo iliyopo Mtaa wa Nyarugusu Shehia ya Pangawe Wilaya ya Magharibi.
Balozi Seif alisema Serikali kupitia Wizara inayosimamia masuala ya Ajira ina mpango wa kuwawezesha Wananchi hasa Vijana kujiendesha kimaisha  katika dhana nzima ya kuwajengea mazingira ya kuchapa kazi kwa vile Vijana ndio nguvu kazi kubwa inayotegemewa na Taifa.
Alisema kazi kubwa inaendelea kufanywa kupitia Taasisi, Jumuiya Washirika wa Maendeleo kwa kushirikiana na Serikali  ya kubadilisha tabia kwa Watu na hasa Vijana kuacha kuendelea kutumia dawa za kulevya.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alizinasihi Familia zenye Vijana wanaotumia au kuathirika na matumizi ya dawa hizo kuacha hulka ya kuwatenga Vijana wao jambo ambalo linaweza kuwazidishia kutumbukia katika janga hilo kwa kukosa ushauri pamoja na msaada.
Balozi Seif alisema katika kukabiliana na tatizo hilo ni vyema kwa Familia hizo kujenga tabia ya kufuatilia kwa kina Vijana wao walioko katika Nyumba za Kurekebisha Tabia kwa lengo la kuwarejesha katika mazingira yao ya kawaida.
Aliwapongeza Vijana hao walioamua kuacha matumizi ya dawa za kulevya kwa hiari yao na kuwataka wahakikishe wanajilinda kwa nguvu zao zote kuwepuka kurejea katika matumizi hayo hatari kwa afya zao.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...