Drug Free Zanzibar (DFA) imeandaa maenyesho ya
Sober House Recovery Art Exhibition. Katika maonyesho hayo vijana wanaoishi katika
nyumba za kurekibishia tabia waathirika wa dawa za kulevya (Sober Houses)
watapata fursa ya kuonyesha vipaji vyao katika fani za uchoraji, ushonaji na
uchongaji wa vitu mbalimbali.
Pia wanajishughulisha mafunzo ya lugha za
kiingereza na kifaransa, yoga, drama pamoja na shughuli mbalimbali za uzalishaji mali .“Sober Houses”
hizi zimesaidia mamia kwa mamia ya vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini kuachana
na matumizi ya dawa za kulevya wakiwemo watu maarufu katika fani mbalimbali.
Lengo la haya yote ni kuwasaidia vijana ili warudi katika mstari na kurudi
katika jamii zao stahiki.
Maonyesho haya yatafanyika katika ukumbi wa
Alliance Franchise Upanga kuanzia tarehe 17 mpaka tarehe 19/10/2012, saa tatu
asubuhi mpaka saa kumi na mbili jioni. Kiiingilio ni bure na wote mnakaribishwa
kushiriki ili kuwasaidia na kuwatia moyo vijana wetu ambao wameamua kuachana na
matumizi ya dawa za kulevya na kuwa mfano bora kwa vijana wenzao ambao bado wanajishughulisha
na matumizi pamoja na biashara ya dawa hizi.
Kwa maelezo zaidi, kusaidia pamoja na ushauri
unaweza kuwasiliana na
ndg. Suleiman Mauly 0782 000426 au
ndg. Alois Ngonyani
0713 334423/0686 334423



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...