Mbunifu wa mavazi wa Kitanzania,Martin Kadinda aliyezoeleka kwa jina la single button amekutana na balozi wa Tanzania New York,Mh. Balozi Tuvako Manongi ofisini kwake jijini New York jana jioni... Martin Kadinda ambaye bado yupo nchini Marekani akihudhulia New York Fashion week, alipata nafasi ya kuzungumza na Mh. Balozi Tuvako Manongi ambaye alimpongeza kwa jitihada zake za kutangaza Tanzania kupitia sanaa ya ubunifu wa Mitindo, pamoja na kujifunza mengi kupitia maonesho makubwa ya mavazi ya New York fashion week,  Mh. Balozi Manongi aliongeza kuwa watanzania wanasimama kifua mbele wakijisifu kutokana na kazi nzuri anazozifanya Kadinda ambazo zimempelekea kualikwa Marekani katika maonyesho ya music on the catwalk, hiyo ni sifa kubwa kwake na kwa taifa lake.. aliongeza kuwa inabidi aongeze juhudi na kutengeneza njia kwa wabunifu zaidi na wasanii wengine kuweza kupeperusha bendera yetu nchi nyinginezo kubwa duniani... Martin kadinda alipata nafasi ya kutia saini kitabu cha wageni pamoja na kupiga picha na balozi na maafisa mbali mbali wa ubalozi jijini New York.  Martin Kadinda aliondoka nchini Agosti 30 kuelekea Marekani ambapo alishiriki maonyesho ya Music on the catwalk Africa New York Fashion week, baada ya hapo amekuwa akihudhuria maonyesho ya New York fashion week akiwa na mwanamitindo Flaviana Matata, Rosemary Kokuhilwa na Millen Magese ambao wao wanaishi New York.
 Martin Kadinda akiwa katika picha ya pamoja na Mh. Balozi Tuvako Manongi Katikati na maofisa wengine wa ubalozi jijini New York City.
Mbunifu wa Mavazi hapa nchini,Martin Kadinda a.k.a single button akipata picha ya pamoja na maofisa wa ubalozi New York City alivyo pata fulsa ya kutembelea na kuongea  nao mawili matatu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hivi kwanini watz hata kama ni watu wa fashion kwanini hatupendi kuvaa kuendana na ofisi uliyopo, jamaa katinga ubalozini na kaptula na hapo ni official trip, naweza nikawa nimekosea lakini ndio hali halisi kwa wasanii wetu na wacheza mpira wetu mtu anakwenda katika event muhimu badala atupie vazi kama suti au la kiofisi mtu anapiga jeans. Tukiangalia kwa wanzetu walio mbele kama kuna kitu official watu wanatupia suti na ukimwona huwezi amini kama ni mchezaji au msanii lakini wakienda sehemu zingine wanaendelea kutupia zile zao za walizozoea. Na ndio maana mpiga picha amelitambua hilo akawakata miguu ili asionekane kama amevaa pensi.

    Nina imani hao staff wana exposure kubwa kuliko huyo bwana Kadinda lakini ona jinsi walivyo vaa japokuwa ukiwakuta nje ya hapo watakuwa wamevaa zile za kimtaani

    ReplyDelete
  2. hivi balozi wa tanzania nchini marekani sio bi mwanaidi maajari? au mimi ndio nimekosea? au amebadilishwa?

    ReplyDelete
  3. Balozi Tuvako Manogi ni balozi kwenye Ubalozi wa kudumu wa umoja wa mataifa,kachukua nafasi ya balozi Ombeni Sefue Katibu mkuu Kiongozi..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...