Timu ya Habari ikisherehekea ushindi wake dhidi ya Tamisemi katika michuano ya SHIMIWI inayoendelea katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro. Habri walishinda kwa bao 15-14
Grace Kingalame wa timu ya mpira wa Netiboli Wizara ya Habari, akiudhibiti mpira mbele ya mpizani wake
Kikosi cha wachezaji wa Netiboli cha Tamisemi kabla ya kuanza mchezo wao na Habari.
Kocha wa Timu ya Netiboli ya Habari , Anna Kibira ( kushoto) akiwa na kikosi chake kabla ya kucheza na Tamisemi, Habari ilishinda mabao 15-14
Patashika kati ya Ardhi ( bluu) dhidi ya Kilimo.
Ardhi walishinda mabao 30-22.
TIMU ya mpira wa netiboli ya Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, imeanza vyema katika michuano ya Shirikishio la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali yanayoendelea Mkoani hapa baada ya kuifunga timu ya Tamisemi mabao 15-14.
Mchezo huo ambao ulikuwa ni wa vute ni kuvute, kila timu ilipania iwezekuibuka na ushindi , lakini wachezaji wa timu ya Habari chini ya Kocha Mkuu , Anna Kibira, walisimama imara kuhakikisha wanapata ushindi muhimu katika mchezo huo wa kwanza.
Hadi mapumziko , Habari ilikuwa mbele kwa mabao 9-7 na kipindi wachezaji wa pande zote walionesha umahiri wa mchezo huo na hadi mwishi wa mchezo Habari iliibuka mshindi kwa mabao hayo.
Wachezaji mahiri wa Habari, Watende Nassor (GA), Grace Kingalame (GS) na Joyce Kunambi (WD) walitumia uzoefu wao ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo huo muhimu uliofanyika juzi ( Sept 24) uwanja wa Jamhuri wa Mjini hapa.
Timu nyingine zilizocheza na kupata ushindi katika michezo hiyo ni pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iliyoibuka na ushindi dhidi ya Mambo ya Ndani kwa kuifunga mabao 32-13, wakati Ras Mtwara iliifunga Viwanda mabao 30-17, nyota wa Mtwaraa katika mchezo huo walikuwa ni Halima Mndolwa na Rehema Mpai.
Mchezo mwingine iliokuwa ni wa vuta ni kuvute ni kati ya Kilimo na Ardhi, ambapo vijana wa Ardhi waliibuna na ushindi wa mabao 30-22, mchezaji Mariam Kungulilo (GS) aliweza kufunga mabao 17 ,wakati mwenzake Kalova Kihwele akipachika mabao 13, ambapo Madini waliifunga Utumishi mabao 28-20 , wakati Ras Singida iliwafunga Mambo ya Nje mabao 49-11.
MCHEZO WA SOKA
TIMU sita za soka ikiwemo ua Idara ya Uhamiaji pamoja na Ikulu, zimewezekufanya vizuri katika mashindano ya michezo ya Wizara na Idara za Serikali ( SHIMIWI) baada ya kuwagaragaza wapindani wao .
Michezo hiyo ya makundi tofauti ilifanyika juzi ( Sept 23) katika uwanja wa Jamhuri wa Mjini hapa, ambapo timu ya Uhamiaji iliweza kuifunga Viwanda bao 5-2 , wakati Ikulu iliifunga Mambo ya Ndani bao 4-1 .
Pia katika kinyang’anyiro hicho, Ras Dar es Salaam, iliishinda Wizara ya Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makzai kwa bao 3-0, Tamisemi kuifunga Ras Arusha bao 1-0 , Osha kuichakaza Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kwa bao 2-0.
Timu nyingine za soka zilizopata ushindi siku hiyo ni Mahakama kuifunga Ras Kagera bao 1-0, Idara ya Utafiti wa madini ( GST) nayo kuifunga Mambo ya Nje bao 1-0 na Hazina kuifunga kwa mbinde timu ya Wizara ya Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo kwa bao 1-0.
KUVUTA KAMBA WANAWAKE NA WANAUME.
TIMU tisa za Kuvuta kamba kati ya hizo sita za wanaume na tatu za wanawake zimefanyavyema katika michezo yao ya kuvuka kamba iliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Jamhuri wa Mjini hapa.
Kwa upande wa wanaume, timu zilizopata ushindi ni Maliasili iliyoishinda Ukaguzi, Hazina kwa kuwatambia TMAA, Uhamiaji iliwavuta wenzao wa Polisi,Makamu wa Rais ( VPO), iliitoa jasho timu ya GST , ambapo Mahakama iliifungia kazi timu ya Haki za Binadamu.
Hata hivyo , tim nyingine zilizoshinda kwenye kinyang’anyiro hicho ni pamoja kwa wanaume ni vijana wa Ikulu waliowashinda wenzao wa Tume ya Sheria.
Kwa upande wa wanawake, Ofisi ya Bunge iliibuka washindi dhidi ya Ras Singida, Ofisi ya Waziri Mkuu iliishinda Afrika Mashariki, Afya iliitambia Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo , Ukaguzi iliizima Ujenzi , GST ilipata ushindi dhidi ya VPO.
Timu nyingine za kuvuta kamba wanawake zilizojipatia ushindi ni Viwanza kwa kuishinda Kilimo, Mifugo kuifunga Mambo ya Nje , wakati vijana wa Hazina walitoka sare ya Ras Iringa.
( Picha na Habari na John Nditi wa Globu ya Jamii).


Safi sana, mashindano ya SHE, ME, WE...! Mbona hakuna HE.
ReplyDelete