Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Amina Masenza (wapili kulia) akifungua rasmi mashindano ya Safari Pool Taifa .Kulia ni Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Ilemela(OCD),Debora Magiligimba.Wengine kutoka kushoto ni Katibu wa chama cha Pool Mkoa wa Ilala, Mohamed Mwarabu, Mwenyekiti wa kamati ya mashindano, Haji Kapulila na Makamu mwenyekiti wa TAPA, Fred Mushi.
Meneja
wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akizungumza na wachezaji wa
Pool (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Safari Pool
Taifa yaliyofunguliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Amina Masenza
katika Hoteli ya Monarch jijini Mwanza jana.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilemela, Amina Masenza akizungumza na wachezaji (hawapo
pichani) wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Safari Pool Taifa katika
Hoteli ya Monarch jijini Mwanza.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari
Lager, Oscar Shelukindo na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pool Taifa,
Fred Mushi.
Waamuzi wa mchezo wa Pool wakiongoza maandamano ya kuingia ukumbini wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Safari Pool Taifa yaliyofunguliwa rasmi jana katika Hoteli ya Monarch jijini Mwanza na Mkuu wa Wilya ya Ilemela, Amina Masenza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...