Mchungaji Dr. Emmanuel Kandusi (kulia) ,
manusura, mwathilika wa saratani ya tezi dume (prostate cancer) na mwanzilishi wa Tanzania 50 Plus campaign yuko
Washington DC kwenye Kongamano (Summit) la saratani ya tezi dume linaofanyika
katika jengo la Maseneta wa Marekani Russell Hall Capitol Hill.
Katika
kongamano hilo ambalo limehudhuriwa na waathilika na wanaharakati wa saratani
ya tezi dume na baadhi ya Maseneta na Wabunge (Members of Congress) unajadiri
pamoja na mambo mengi umuhimu wa kutoa elimu katika jamii juu ya saratani ya
tezi dume na umuhimu wa kutoa tiba ya kisasa kwa watu wote na mahali popote.
Kongamano linalohudhuriwa na washiriki takribani mia moja, umeandaliwa na
shirika la hiari Prostate Health Education Network la Marekani na lenye makao
makuu huko Boston. Shirika hilo linakazia “Knowledge is the best defense
against prostate cancer”.
Kongamano liligundua kuwa kwa kutoa elimu katika jamii
utawezesha kupunguza magonjwa ya saratani (prevention is better than cure) kwa
watu wengi. Watu wakielimika na kupata elimu juu ya hali hatarishi, uuhimu wa
kubadili maisha yao kwa kula vyakula asilia, kufanya mazoezi, kujiepusha na
utumiaji wa tumbaku wa aina yote, kupiga vita unene hatarishi itapunguza sana
watu kupata saratani.
Hii itaokoa nguvu kazi na kuokoa pesa nyingi ambazo
zinaweza kutumia kwa maendeleo mengine. Katika picha ni Dr. Kandusi akimkabidhi
magazeti ya MAN Rais na Mwanzilishi wa Prostate Health Education Network Ndugu
Thomas Ferington. Ndugu Farrington naye ni manusura, mwathilika na mhanga wa
saratani ya tezi dume.



Jamani hapa tuna "hero" ambaye ingefaa taifa limtambue. Kwa nini naye asipewe tuzo! Ahsante kutupatia elimu saratani ya tezi dume na pia kutuwakilisha hata uendapo huko ughaibuni. Mungu akubariki!
ReplyDelete