Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi madawati yaliyotolewa na Kampuni ya African Barrick Gold kwa shule ya Msingi Minazi Mirefu,iliyopo eneo la Kipawa Banana,Jijini Dar es Salaam leo.anaesaidiana nae ni Mkurugenzi wa Mahusiano ya Serikali wa Kampuni ya African Barrick Gold,Emmanuel Ole Naiko na aliesimama nyuma ya Mh. Lowassa ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira na Mbunge wa Jimbo la Segerea,Mh. Makongoro Mahanga.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (katikati),Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga (kulia),Mkurugenzi wa Mahusiano ya Serikali wa Kampuni ya African Barrick Gold,Emmanuel Ole Naiko (pili kushoto) na Meneja Mawasiliano wa African Barrick Gold,Nector Pendaeli (kushoto) wakiwaangalia wanafunzi wa Shule ya Msingi Minazi Mirefu,iliyopo eneo la Kipawa Banana,Jijini Dar es Salaam leo waliokuwa wameketi kwenye sehemu ya Madawati 500 yaliyokabidhiwa leo na Kampuni ya African Barrick kwa shule hiyo.Hii ni sehemu ya Jitihada zinazofanywa na Diwani wa Kata ya Kipawa,Bi. Boma Kaluwa kwenye kuinua maendeleo ya kata yake.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimia na baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Minazi Mirefu,iliyopo eneo la Kipawa Banana,Jijini Dar es Salaam leo wakiompokea kwa shangwe na bashasha tele.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...