Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Theresia Huvisa akizungumza na wandishi wa habari jijini Arusha leo kuhusiana na maandalizi ya mkutano wa 14 wa Mawaziri wa Mazingira kutoka barani Afrika Tanzania ikiwa mwenyeji wa mkutano huo.
Watoto wakifanya mazoezi ya wimbo maalum watakaoimba kesho kwenye mkutano wa 14 wa mawaziri wa mazingira barani Afrika mbele ya Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) nchini Tanzania Mh. Theresia Huviza.
Harriet Macha kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa(kushoto) akitoa maelezo mmoja wa wadau wa mazingira aliyefika katika banda la Umoja wa Mataifa lililopo katika jengo la AICC utakapofanyika mkutano wa 14 wa mawaziri wa Mazingira.
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu aktioa maelezo kwa mmoja wa wadau ya namna Umoja wa Mataifa inavyoshirikiana na Serikali ya Tanzania katika utunzaji wa Mazingira kupitia mpango wa mazingira (UNEP) uliopo chini ya Umoja wa Mataifa.
Banda la ROA OZONE ACTION PROGRAMME chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais na UNEP wakitoa maelezo katika kutunzaji wa mazingira kwa wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...