Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwasili katika ukumbi wa MNelum Pokuna Mahinda Rajapaksa kuhudhuria ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 58 wa chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) uliofunguliwa leo na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa. Aliye pembeni yake ni Mjumbe wa CPA Tawi la Tanzania na Mbunge wa Kigoma Mhe. Zitto Kabwe.
Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa akihutubia Maspika, Wabunge na maafisa zaidi ya 850 kutoka Mabunge ya nchi wanachama jumuiya ya madoloa wakati wa ufunguzi rasmi wa mkutano huo.
Spika wa Bunge. Mhe. Anne Makinda akifuatilia kwa umakini ratiba ya ufunguzi wa Mkutano wa 58 wa chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) kabla ya ufunguzi rasmi leo Mjini Colombo Sri, Lanka, aliye kushoto kwake ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pande Ameir Kificho na Mhe. Zitto Kabwe na aliye kulia ni Mhe. Mussa Azzan Zungu. Mkutano huo umefunguliwa rasmi leo na Rais wa Nchi hiyo Mhe. Mahinda Rajapaksa.
Spika wa Bunge. Mhe. Anne Makinda akiteta jambo na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pande Ameir Kificho pamoja na Mhe. Zitto Kabwe wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 58 wa Chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) leo Mjini Colombo, Sri Lanka. Mkutano huo umefunguliwa rasmi na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa. Wa Kwanza kulia ni Afisa dawati wa CPA tawi la Tanzania Ndg. Said Yakubu.
Mhe. Zitto Kabwe akiteta jambo na Mbunge toka Uganda (hakufahamika jina mara moja) pamoja na Spika wa Bunge la Malawi Mhe. Henry Chimundu Banda (katikati) mara baada ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 58 wa CPA unaofanyika nchini Sri Lanka. Kulia ni Mhe. Hamad Rashid Mjumbe wa CPA tawi la Tanzania.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akishangaa jambo wakati wakiwa katika mazungumzo na Spika wa Kenya Mhe. Kenneth Marende mara baada ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 58 wa CPA unaofanyika nchini Sri Lanka.
Wajumbe wote wa Mkutano wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi rasmi leo.Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Huo mkoba wa Mh. Zito mbona mtihani!!! Kama wa kike vile!!!

    ReplyDelete
  2. Sorry to say it but you would be hard pressed to find attractive politcians anywhere in the world

    ReplyDelete
  3. 2015 ni karibu wakati wakinamama umeshafika.Je Tanzania iko tayari kuongoza na wanawake? Dr. Migiro pamoja na wakinamama wegeno mbona wako kimya?

    ReplyDelete
  4. Mdau Anonymous wa Thu Sep 13, 02:43:00 AM 2012

    ....2015 ni karibu wakati wakinamama .....je Tanzania iko tayari kuongozwa na wanawake?

    JIBU NI HAPANA:

    Wanawake katika Dunia na Afrika baaado kabisa angalieni mofano miwili hapa chini Maraisi wanawake Afrika:

    1.Mama Joyce Banda,(MALAWI)

    Ana utawala wa jazba alipoingia Ikulu wiki ya kwanza,

    -Mkuu wa Polisi hana kazi, Gavana wa Benki kuu hana kazi, na wazito lukuki nyumbani timua timua!.

    -Mwezi mmoja mbele anaigeukia Tanzania anadai umiliki wa Ziwa Nyasa wakati je waliomtangulia hawakuwa wanaona hili?

    2.Mama Ellen Johnson Sirleaf(LIBERIA)

    -Kampuni kubwa ya Usafirishaji Mafuta Mkurugenzi Mkuu anamchagua mwanaye !

    Je, wanawake wanasomeka kuwa Maraisi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...