Hifadhi ya Serengeti ni eneo kubwa la savana na misitu katika Tanzania ya kaskazini hasa katika mikoa ya Mara na Arusha ikipakana na Kenya. Eneo lake ni 14,763 km² na kijiografia kipande kidogo kinaendelea ndani ya Kenya katika  Hifadhi ya Masai Mara.
Kuna idadi kuba ya wanyama wa pori. Serengeti pamoja na Masai Mara inajulikana hasa kwa uhamisho wa kila mwaka wa zaidi ya milioni moja ya nyumbu wanaovuka mto Mara. Kuna pia aini nyingi nyingine za wanyama kati yao "watano wakubwa" wanaovuta watalii hasa ya anitembo, simba, chui, fisi, kifaru na nyati.
Karibu na mwezi Oktoba, karibu herbivores (yaani wanyama wanaokula majani badala ya nyama) milioni 2 husafiri kutoka milima ya kaskazini kuelekea nyanda za kusini na kuvuka mto wa Mara katika harakati za kusaka malisho wakati wa mvua katika kile kinachojulikana kama annual animal migration. 
Katika mwezi wa Aprili hurejea kaskazini kwa kupitia magharibi, na kwa mara nyingine tena kuvuka Mto wa Mara na kurudi Tanzania. Jambo hili  huitwa "Circular migration" yaani uhamiaji mviringo. Nyumbu zaidi ya 250,000 hufa wakiwa safarini kutoka Tanzania kwenda katika mbuga ya wanyama ya Masai Mara,  ambayo ni jumla ya maili 500. Vifo hivi mara nyingi husababishwa na wanyama wakali wanaowawinda, maradhi au uchovu.  Uhamiaji huu umeonyeshwa katika filamu na programu nyingi za televisheni kote duniani na kivutio kikubwa cha utalii.

Ankal akiwa katika kingp za Mto Mara ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kushuhudia uhamaji wa wanyama
Magari kibao yaliyobeba watalii yamesimama pembeni ya Mto Mara tayari kujionea wanyama wakivuka katika hiyo annual anima migration
Wanyama wakijikusanya kabla ya kuvuka Mto Mara
Watalii wakisubiria kurekodi tukio hili la kila mwaka
Wanyama wakiendelea kusubiri muda muafaka wa kuvuka
Ukiandalia kwa makini chini kushoto sio mwamba bali ni moja ya mamba wengi wanaosubiri mlo wa wanyama wataovuka hapo Mto Mara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Tuletee picha zaidi Bro Michuzi.Lakini kwenye http://sevennaturalwonders.org/category/africa/ hiyo Migration inashika nafasi ya nne kwa maajabu Afrika, Watanzania tuendelee tuendelee kuvipigia kura vivutio vyetu,sioni mantiki ya Red Sea Reef kuongoza

    Msimamo ni kama ifuatavyo:

    1:Red Sea Reef
    2:Mount Kilimanjaro
    3:Sahara Desert
    4:Serengeti Migration
    5:Tsingy de Bemaraha
    6:Avenue of the Baobabs
    7:Ngorongoro Crater

    Mdau David V

    ReplyDelete
  2. Masikini roho zetu Watanzania, hata wale wenye uwezo hawaendi huko kuona maajabu yao.

    Wanafaidi wazungu tu.

    ReplyDelete
  3. Michuzi pitia pia Ngoro ngoro karibu na Oldvai (Oldpai) kuna mchanga unaohama (shifting Sands) nilipita hapo jana ni kitu kinachohitaji kutangazwa weka kwenye blog halafu wabeba box wapigie debe kwani wizara imeshindwa kazi ya kutangaza vivutio hivyo. tuwatumie watani wabeba box kufanya hilo

    Observer

    ReplyDelete
  4. Kaka Michuzi kundi hilo limepungua sana sana na barabara ikipita tu hapo ndo kabisa hiyo starehe ya kuhama wanyama itakwisha. Pili katika pori la Simanjiro kuna uwindaji uliopitiliza sidhani kama wizara inajua madhara yake. maafisa wanyama pori huko wananeemeka tu bila kujali madhara yake

    ReplyDelete
  5. Assalama Leko zako Mjomba Muhidin Issa Michuzi!

    Unafiti kote kote ankali, yaani upo mbugani hukooo kama vile askari wa wanyama pori!

    Kweli Michuzi kifaa sana!

    ReplyDelete
  6. Mwaka huu wamesema hawavuki bongo njaa imekithiri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...