Waziri wa uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe na ujumbe wake wapo Berlin kuanzia  15 hadi 19 sept, 2012 kwa ziara ya kikazi. Moja ya matukio muhimu ni kusainiwa Mkataba wa Ushirikiano wa Usafiri wa Anga (Bilateral Air Services Agreement - BASA) baina ya nchi hizi mbili tarehe 17 Sept. Aidha, tarehe 16 sept, Mhe. Waziri na ujumbe wake walitembelea maonyesho ya Kimaitaifa ya sekta ya Usafiri wa Anga yaliofanyika jijini Berlin ambapo  kwa nyakati mbalimbali, Mhe. na ujumbe wake wanakutana na wafanyabiasha na wawekezaji mbalimbali hususani katika sekta ya usafiri wa anga, reli na majini.

 Mhe. Waziri akiwa ndani ya moja ya ndege iliyokuwepo katika maonyesho hayo.
 Mhe. Waziri akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa ndege za Airbus, nchini ujeruman (hayupo pichani) pembeni yake ni Mhe. balozi wa tz Berlin.
 mhe. waziri akiwa na Balozi wa tz Berlin Mhe. Ahmada R. Ngemera (kushoto) na Afisa wa Wizara ya mambo ya Nje, Ali Ubwa Mussa (Kulia).
  Mhe. Waziri na ujumbe wake wakiwa katika maonyesho ya Sekta ya usafiri wa Anga mjini Berlin.
Mhe. Waziri na ujumbe wake wakiwa katika Majadiliano na Uongozi wa Sekta ya Usafiri wa Anga, Germany.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Afadhali umeenda mwenyewe kununua ndege inayofaa badala hao jamaa zako wachakachue. Hongera sana jembe letu.

    ReplyDelete
  2. Mwakyembe is hardworking and freedom fighter..Tumpe nafasi ataleta mabadiliko makubwa sana-Hana mambo ya itikadi za chama chake wala nini-Yeye hatetei madudu hata kama niya wenzake. Kero ya Mizigo yetu bandari kucheleweshwa na kuwekewa mizengwe ya kutoa Rushwa Tusaidie Mheshimiwa waziri. Pale bandarini kuna uhuni uhuni sana. Safisha pale mkuu. Nakuomba passport za bongo zinacheleweshwa mno mpaka utoe kitu kidogo wakati Passport ni Haki ya Kila raia wa Tanzania,Mpige Jerk Nchimbi kalala Kidogo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...