Balozi wa heshima wa Anuani za Makazi duniani Prof Anna Tibaijuka (MB) (Wa pili kushoto) akisoma anuani ya makazi ya jengo la Mawasiliano muda mfupi baada ya kuizindua. Kulia ni Prof. Makame Mbarawa Waziri wa Mawasiliano ,Sayansi na Teknolojia (MB) na Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe (MB) wakishuhudia uzinduzi huo. (Kulia) ni Prof John Nkoma Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano akitoa maelezo kuhusiana na mradi wa Anuani za makazi nchini Tanzania .
Mh. Prof. Anna Kajimulo Tibaijuka Balozi wa Heshima wa Anuani za Makazi duniani muda mfupi baada ya kutambulishwa rasmi kwa vyombo vya habari nchini. Katika hafla hiyo Mh. Balozi, Prof . Anna Tibaijuka aliahidi kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha kuwa wakazi wote duniani wanapata anuani za makazi.
Mh. Balozi. Prof. Anna Tibaijuka akimkabidhi Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Makame Mbarawa anuani iliyo katika mfumo mpya wa anuani ya makazi kwa ajili ya wizara yake. Mfumo mpya wa Anuani za Makazi unaonyesha kanda, mkoa, wilaya, kata, mtaa na namba ya nyumba hivyo kurahisisha ufikishaji wa huduma za posta kwa wananchi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Camilius Membe (MB) akitoa nasaha kwa balozi mteule wa kimataifa wa anuani za makazi (hayupo pichani) mara baada ya kutambulishwa rasmi kwa wananchi. Mh. Membe kwa niaba ya watanzania alimtakia heri Mh. Balozi. Prof. Anna Tibaijuka katika kazi yake hiyo na kumuhakikishia ushirikiano kutoka kwa watanzania.
Mh. Balozi. Prof. Anna Tibaijuka (MB) akifanyiwa mahojiano na wanahabari walihudhuria kutambulishwa kwake (kushoto) ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. Makame Mbarawa akishuhudia. Mradi wa mfumo mpya wa anuani za makazi unasimamiwa na Wizara ya Mawasilisano, Sayansi na Teknolojia chini ya Sekretarieti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Picha ya pamoja na Mh. Balozi wa kimataifa wa anuani za Makazi.


.png)
.png)
.png)
.png)
.png)
.png)
Hapa serikali wanasema kila mwananchi anapaswa kuwa na anuani ya makazi lakini mie navyoona katika utekelezaji wa mpango huu lazima watakutana na changamoto ya wakazi wengi wa mjini wanaishi kwenye nyumba za kupanga na wengi wao ni wanahamahama kutokana na mabadiliko ya kiuchumi yatokanayo na upandaji holela wa kodi, sasa katika situation kama hii sijui wamejiandae kupambana na changamoto hii.(najua wakati wanajipanga walijiangalia wao kwa kuwa wengi wana makazi ya kudumu hawakufikiria nje ya box)
ReplyDeleteMdau Igwamanoni wa Itabagumba
Mtoa maoni wa kwanza ni MBUMBUMBU. Ni anwani ya makazi si anwani ya mtu. Akihama anaiacha anwani yake ya awali. Atakapoenda ataikuta anwani mpya. Kama mfumo wa utambulisho wa taifa utakuwa umeanza kazi, atatakiwa kwenda mamlaka husika na kubadili anwani
ReplyDelete