Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi kuashiria kuzindua rasmi ujenzi wa Daraja la Kigamboni katika hafla iliyofanyika huko Kurasini jijini Dar es Salaam leo mchana.Kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli na wapili kulia ni mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhani Dau.NSSF itatoa asilimia 60 za ujenzi wa daraja hilo na serikali itatoa asilimia 40
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati akiongea na Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni uliofanyika huko Kurasini jijini Dar es Salaam leo mchana.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati akiongea na Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni uliofanyika huko Kurasini jijini Dar es Salaam leo mchana.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik
Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli akimpa maelezo
Raid Dtk.Jakaya Mrisho Kikwete juu ya Ujenzi wa Daraja la Kigamboni wakati wa
hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa Daraja hilo ulofanyika Kurasini jijini Dar ea
Salaam leo mchana.
mh raisi wangu Kikwete me naona hawa jamaa kila siku wanakuletea siasa kwenye ujenzi wa hili daraja maana kila siku linaongelewa mara kuwekwa jiwe la msingi mara kuanza kujengwa mara sasa kuzinduliwa wakati hatuoni likijengwa kwa kasi kama ilivyosemwa. Mh raisi nakuomba usikubali tena wakuite kwenye hii ishu ya daraja waambie tu wakuite likikamilika maana nadhani hawajui cheo cha urais kinavyotakiwa kuwa respected...mdau kigamboni future resident
ReplyDeleteBig up.... Hongera sana serikali na nssf kwa juhudi..... I pray that ujenzi uende bila tatizo.....
ReplyDeleteAngalizo, ile haya mabarabara na madaraja ya 'Magufuli' isiwe Dar tu, serikali ikumbuke Tanzania ni kubwa na Tanzania yote inahitaji 'mabarabar', 'madaraja', na pia 'Mareli' ya TAZARA na TRL kwenda mikoani pia iboreshwe ili kuchangamsha uchumi na kuunganisha masoko kwa usafiri wa hakika wa kila aina.
ReplyDeleteMdau
Mwisho wa Reli
Tanganyika
Barabara Msata-Bagamoyo, Ya Kuelekea Morogoro, Dar kuelekea Bagamoyo na sasa Daraja la Kigamboni. Mungu ibariki Tanzania. Wape afya njema na upeo zaidi wale wote wanaochapa kazi kwa dhati na si kwa chati.
ReplyDeleteTungekua na ''MAJEMBE''haya matatu(Magufuli-Miundombinu,Mwakyembe-Usafirishaji na Kagasheki-Maliasili na utalii)kama ishirini hivi Hakyamungu Tungekua mbali isivyoelezeka...Mungu wabariki hawa mawaziri watatu waendelee kuchapa kazi sio hao wanaoendekeza propaganda za kisiasa tu na utendaji ziro.
ReplyDeleteWewe unaemsifia magufuli jembe, JEMBE HAPA NI KIKWETE NA DR DAU, huyo magufuli wenu mbona aligoma daraja lisijengwe ? leo anasifiwa magufuli ! mbona mnamsahau Dr Dau!
ReplyDelete