Spika wa Bunge akisisitiza Jambo wakati akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge Mjini Bagamoyo.
katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akimkaribisha Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda kufungua rasmi Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge Mjini Bagamoyo.
Mkurugenzi wa Maktaba na Utafiti katika Ofisi ya Bunge Ndg. Kileo Nyambele akitoa neno la Shukrani kwa Mhe. Spika mara baada ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge.
Watumishi wa Bunge wakimsikiliza Mhe. Spika wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge Mjini Bagamoyo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Kulia), katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah (katikati) na Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Ofisi ya Bunge Ndg. Angumbwike Ng'wavi wakiimba wimbo wa Mshikamano wa TUGHE kabla ya Ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Barza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge, Mjini Bagamoyo.
Kamishna wa tume ya Utumishi wa Bunge Mhe. Godfrey Zambi akiteta jambo na Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda mara baada ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge Mjini Bagamoyo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiagana na watumishi wa Bunge mara baada ya kufungua mkutano wa mwaka wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika Mjini Bagamoyo.
Viongozi wa TUGHE kutoa Taifa, Mkoa wa Dodoma na Ofisi ya Bunge wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi mara baada ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge Mjini Bagamoyo.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa mwaka wa Baraza hilo Mjini Bagamoyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Sielewi kwa nini hao wafanyakazi wa Bunge wafanyee mkutano wao Bagamoyo wakati katika ofisi zao kuna kumbi za kutosha tu kufanyia mkutano huo....... viongozi jaribuni kubana matumizi hizo per diem mnatuchosha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...