Mkurugenzi wa Kampuni ya Edge Entarteinment Co Limited Bw. Edwin akizungumza na waandishiEdge Entertainment Co Ltd imeandaa tamasha kubwa la muziki wa dansi linalojulikana kwa jina la Tanzania Live Music Festival litakalofanyika kwa muda wa siku mbili za Septemba 28 na 29 mwaka huu, katika viwanja vya Leaders Club kuanzia saa 10.00 alasiri na kuendelea. Wengine pichani toka shoto ni Mafumu Bilali Bombenga, John Kitime, Dada, Hartman Mbilinyi na King Makosa
Tamasha hili lina lengo la kukuza muziki wa dansi nchini Tanzania, kukusanya fedha kukisaidia Chama cha Muziki wa Dansi (chamudata) kiweze kujiendesha kwa ufanisi. Kuchangia mfuko wa sanaa ulio chini ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).
Tamasha hili litajumuisha bendi mbalimbali za muziki wa dansi nchini na litakuwa likifanyika kila mwaka, na tunatarajia kwa miaka ijayo kukutanisha bendi mbalimbali nchini na kualika bendi au wanamuziki wakubwa kuja kushiriki toka nje ya Tanzania.
Katika kufanikisha tamasha tumemchagua mcheza filamu Jackline Wolper kuwa Balozi wa tamasha hili kwa mwaka 2012.
Siku moja kabla ya tamasha 27/9/2012 kutakuwa na mafunzo ya siku moja kwa wanamuziki kuhusu hati miliki yatakayotolewa na COSOTA.
Wadhamini wetu ni :TIMES FM RADIO, GLOBAL PUBLISHERS, BUSINESS TIMES, VODACOM TANZANIA



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...