Mfanyakazi katika Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Adolf Ndyeabura (aliyevalia fulana ya Yanga kulia) akiwaonyesha kocha wa timu ya Yanga, Thom Sainfiet, na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo jinsi bia zinavyopikwa juzi Alhamisi wakati timu hiyo yenye maskani yake katika mtaa wa Jangwani jijini, ilipofanya ziara yake katika kiwanda cha TBL kilichopo Ilala jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe (kushoto) akiwa na beki mpya wa timu ya Yanga, Mbuyu Twite (katikati) na Msemaji wa timu hiyo, Louis Sendeu Alhamisi wakati timu hiyo yenye maskani yake katika Mtaa wa Jangwani jijini Dar es Salaam ilipofanya ziara katika kiwanda cha kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Anayeonekana nyuma yao ni kocha wa timu hiyo, Thom Sainfiet.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe (kushoto kabisa) akiwa na baadhi ya viongozi wa vitengo mbalimbali vya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) pamoja na wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa timu ya Yanga juzi Alhamisi wakati mabigwa hao wa Kombe la Kagame walipotembelea kiwanda cha TBL kilichopi Ilala jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa timu ya Yanga pamoja na benchi la ufundi la timu hiyo na baadhi ya viongozi wa timu wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wanawake katika Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) juzi Alhamisi wakati timu hiyo ilipofanya ziara kiwandani hapo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...