Kichwa cha treni pamoja na mabehewa sita ya awamu ya kwanza,yakisubiri kufanyiwa majaribio kwa  Safari zitazoanzia Station ya Dar es Salaam Mpaka Ubungo mnamo mwezi wa kumi. Majaribia hayo yameongozwa  na Naibu Waziri wa Uchukuzi,Mhe. Dk Charles Tizeba(Mb) ambaye alipanda treni hiyo kuanzia Station Dar es Salaam Mpaka Ubungo.Serikali imetumia kiasi cha Sh. Bil 4.75 kwa ajili ya ukarabati wa njia,injini na mabehewa.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba(Mb),akipanda treni wakati wa majaribio ya Mabehewa sita ya treni kati ya mabehewa kumi na mbili yanatogemewa kutumika na Shirika la reli Tanzania(TRL). Treni hizo  zitakayofanya safari zake kutoka Station Dar es Salaam mpaka Ubungo,mapema mwezi wa Kumi.
  Baadhi ya wananchi wakipanda katika behewa moja kati ya Sita yaliyofanyiwa majaribio mapema leo kutokea Station mpaka Ubungo(km 12).
 Mchuma huo unaondoka
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania(TRL) wakiwa na furaha ndani ya mojawapo ya mabehewa yaliyofanyiwa majaribio leo abubuhi.
 Abiria wa majaribio

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 34 mpaka sasa

  1. Ni vema kuthubutu kuliko kusema haiwezekani. Naamini hili litawezekana, na hata kama litakwama credits zinabaki palepale. Kazi nzuri (endapo tu haikugeuzwa mradi wa mfukoni)!

    ReplyDelete
  2. mhhh my country,, so sad

    ReplyDelete
  3. Lakini pamoja na yote kweli hata kusafisha hicho kituo cha kuanzia na kuweka standard imekuwa shida? kweli mtaanza safari hizo kwa hali hiyo na taka zote hizo hapo chini? Kwanini usafi usizingatiwe? Hata mkifungua kuwe na heshima na watu wajue ni kitu cha kuheshimika siyo vurumai tu....!!

    ReplyDelete
  4. Nyie pondeni tu, mlikimbilia kule kuliko pikwa tayari, na mkakaa kula tu,nyamafu nyie.Lakini punde skin head wakiwabagua tu, tayari kilio -o mimi kwetu sikuua ,kama ndo hivi ,nitarudi kwetu,mara o,africa kuzuri bwana hakunyanyasi mtu.Nyie hao hao o kuchafu !!! sasa tuwaelewe je ??? cheki viti vya treni vilivyotulia ,kabla havijaanza kuchorwa chorwa au kuchanwa na viwembe.Kweli ,wakati mwingine sisi ni choo ile babu kubwa.Lakini, iko dalili ya kuuona mwezi.Zebedayo msema kweli

    ReplyDelete
  5. Haya ndio maendeleo

    ReplyDelete
  6. hiyo biashara ingeachiwa private sector. Kwaattitudes za Wabongo dhidi ya vitu vya serikali, watauwa hiyo biashara mda si mrefu.

    ReplyDelete
  7. Tukiacha ushabiki serikali inabidi ipongezwe kwa hili na we need to take this as a way forward toward electric-train..but usimamizi uwe makini na endelevu usiishie kwa mwakyembe tu..

    ReplyDelete
  8. Kuhusu uchafu tusimlaumu mtu kwasababu sisi watanzania ndio wachafu.

    ReplyDelete
  9. Nashauri wangefikiria kuweka viti cichache ili kupata roooms za ajili ya kubeba abiria wengi.Ingawa mimi ndo 'Geneous' Mwakyembe na wenzake ningeshauri waweke viti vya kuangaliana ili katikati wasimame watu wengi zaidi.Pili katika Dar masterplan reli ilitakiwa iiishie Wazo Hill.nadhani ni wakati muafaka ili lifikiriwe bila kujalai kama kuna watu wamejenga ndani ya njia ya reli

    ReplyDelete
  10. Big up Zebedayo msemakweli

    ReplyDelete
  11. Sasa kituo chenyewe kichafu hakina mpangilio watu wanapanda kiholela madirisha ukiwacha wazi upepo ukifunga ni kama upo ndani ya contena la mizigo

    hivi walishindwa kuweka madirisha ya vioo?

    Nina imani huo sio mtaji wa mtu binafsi kama ilivyo kituo cha mabasi ubungo

    jengeni vituo vizuri na vidumishwe kwa usafi

    ReplyDelete
  12. Dar Metro, oyeee!!

    ReplyDelete
  13. yaani namuunga mkono mdau aliesema hiyo biasha iachiwe private sector kabisaa ndo itadumu alafu jamani hayo madirisha ya treni na joto la dar Mungu wangu mpka ufike ubungo kazi ipo.. Hongera sana serikali ya J.k hapo kweli mmethubutu nadhani mtaweze pia..

    ReplyDelete
  14. Jamani BREKI.. BREKI zimo???
    Tusije kurudi tena kwenye maafa ya kitaifa yasiyoisha kila siku...oh!!

    ReplyDelete
  15. Ninyi mnaoponda ni wakati wenu sasa kurekebisha !

    1.Wa Majuu mnaotucheka na kukebehi jitihada zetu ni wakati wenu sasa mchangie kinachowezekana ili hali iwe bora zaidi!

    2.Mliopo hapa Tanzania, ni wakati wenu sasa angalau hata msipofanya usafi kwa vitendo mchangie mawazo!

    3.Sisi tumeanza ninyi mmalizie, sio kulaumu na kudharau!

    ReplyDelete
  16. Hongera!

    Bongo tambarale hali ndio hiyo inaanza kuimarika dege linaanza kuruka!

    Wa Majuu tunafanya maandalizi ili mje kupanda Matreni yetu huku Bongo Tambarale mliojengewa na Mababu zenu badala ya kupanda matreni kwa manyanyaso ugenini.

    Tunajua wengi meshazoea maisha ya Matreni mmelemaa sasa tunawaandalia usafiri Jijini mkifika mtapewa Vitambulisho mtumie ninyi sisi tutaendelea na usafiri wa Mabasi na foleni za barabara msizoweza ninyi!

    Hamjui walilipia kodi mababu zao wakajenga?

    ReplyDelete
  17. Heee Dar-Ubungo?

    Sio Ubungo-Posta?

    Kwani Ubungo ni nje ya Dar?

    ReplyDelete
  18. USAFI!!!

    Sehemu za kujisaidia pande zote mbili yaani stesheni kuu na ubungo, VYOO vipewe kipaumbele cha USAFI.
    Sivyo vitageuka mazalio ya magonjwa yanayotokana na uchafu.

    MAPATO!!!

    Mdau wa kwanza kagusia. Pamulikwe tochi hapo ili pajiendeshe itakavyowezekana. Yaani tuwabane wahusika hizo hela zieleweke.

    ReplyDelete
  19. Wabongo sijui tkoje! viti hivyo vitachanwa na treni kuchorwa na makerpen muda si mrefu, sembuse mali ya serikali lol! Haya kila la heri isiishie majaribio.

    ReplyDelete
  20. hawa wanaoponda shughuli hii wana maslahi yao binafsi kuhusu usafiri wa daaladala hapo Dar. Unajua kuna watu huwa hawapendi mafanikio ya kiujumla ya maendeleo ya raia. Kwa hiyo hao wanaoponda wanajua kuwa watapoteza mapato kutokana na huduma hiyo ya treni

    ReplyDelete
  21. Wa Majuu mnadai hamtaki kurudi Bongo kwa kuwa huko mliko kuna usafiri wa Matreni.

    Matreni ndio haya tumewaandalia karibuni nyumbani Tanzania mje mshiriki ujenzi wa nchi!.

    Haya sasa kila kitu chini ya jamvi ndani ya Bongo,,,mpo hapo?

    ReplyDelete
  22. Hongera sana!

    Wanaobeza wajinyonge!

    Walau,

    1.Tumethubutu,
    2.Tumediriki,
    3.Tumeweza,
    4.Na tunasonga mbele!

    Je Bandugu tuache unafiki na dharau, hivi miongo kadhaa iliyopita tuliyaona haya?

    ReplyDelete
  23. Mnabeza nini Watanzania?

    Mnaobeza acheni dharau kabisa hapa!

    Tazameni mabehewa mazuri tu, viti vizuri makava ya ngozi n.k

    Mnachotakiwa mnaobeza ni kutoa mchango wenu badala ya kuwa 'domo wazi' mchango wa jinsi hali hiiitakavyo lindwa ili ubora udumu na hali iimarike zaidi!

    ReplyDelete
  24. Mnabeza nini Watanzania?

    Mnaobeza acheni dharau kabisa hapa!

    Tazameni mabehewa mazuri tu, viti vizuri makava ya ngozi n.k

    Mnachotakiwa mnaobeza ni kutoa mchango wenu badala ya kuwa 'domo wazi' mchango wa jinsi hali hiiitakavyo lindwa ili ubora udumu na hali iimarike zaidi!

    ReplyDelete
  25. Wewe unaodai chini pachafu kama umeona unangoja nini?

    Si ungedamka alfajiri na fagio lako hadi Stesheni ya Treni ukafanye usafi?

    Wewe unafikiri nchi inajengwa na nani kama sio wewe Mwananchi?

    Unafikiri atakuja Mkazi wa Kigali nchini Rwanda aje akufagilie wewe?

    Kule Wananchi wanafagia kwa ridhaa yao wenyewe kama mchango wa Ujenzi wa Taifa, kalaga baho!

    ReplyDelete
  26. Tauche tabia ya 'NAFSI LAWWAMMA' tuwe na mwenendo wa 'NAFSI MUTUMAINA' angalieni wajinga wanavyo toa kejeli.

    Kama hizi ni jitihada za kuleta hali bora nchini kwa nyie wakazi wa Gongo la Mboto na Mbezi-Kimara ambao mlikuwa mnawacheka wa Mbagala kwa kupandia madirishani kwenye mabasi na ninyi sasa mnapanda hivyo hivyo!

    Sasa mnataka iweje?

    ReplyDelete
  27. Nyie mnaotoa dharau ndio wapanda mabasi madirishani wakazi wa Mbagala, Gongo la Mboto na Mbezi-Kimara!

    Bora watoe hao wa Mbagala reli haipiti kwao sasa nyie wa Mbezi-Kimara na Gongo la mboto si ndio msaada huo?

    ReplyDelete
  28. Nauli ni sh ngapi jamani? nimeipenda .big up.TRl .mwakyembu juuuuuu.

    ReplyDelete
  29. Miunda

    Mi namshauri waziri husika afavye anavyo weza kuweza kuondoa uwoza huo wa matrein mabovu.

    Kama upo wezekano afanye anavyoweza atafute wawekezaji,usafiri huu waachiwe watu binafsi au mashika binafsi ili wauendeleze,watafute mtu kama mwenye company ya Virgen,aje tuunganishie mikio yote kwa train za kisasa.

    itasaidia kukuza uchumi kwa haraka pia baadhi ya mikoa kufua masoko ya biashara kwa usafiri wa uhakika na wa haraka.

    Mdau Miunda.

    ReplyDelete
  30. ni muda muafaka tuanze kupongeza pale jambo zuri linapofanyika na tutoe mawazo ya namna ya kuboresha. hii ni njia sahihi katika kupunguza msongamano wa magari na pia kupunguza udhia wa usafiri kwa hiyo njia. sasa changamoto ni namna ya kufanya lidumu na kukidhi jukumu lilopo

    ReplyDelete
  31. Hongera kwa Mwakembe...
    Mchaka chaka uendelee...

    tunataraji mengi kutoka kwako.

    ReplyDelete
  32. Mlikuwa wapi nyakati zote hizi? Fanya Udhubutu, Reli ipandishe hadi Wazo Hill. Compensations zimetafunwa miaka mingi kupisha extension ya reli kutoka ubungo. Ila kwa Ufisadi wetu!!!!Kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  33. @ zebedayo.
    The thing is uchafu unaonekana hapo, walio nje ya nchi ofcourse ni lazima waseme, kwani hata kufanya usafi tanzania inahitaji mwekezaji? ni vyanzo vya magonjwa hivyo! system ndio mbaya , that's it.

    ReplyDelete
  34. Hapa DSM kuna makabila 300 wengine wametoka vijijini hata vyoo hawakuacha huko, kaenda sekondari, wanajisaidia vichakani kaingia chuo kikuu cga DSM kusoma kile choo pale College of Arts harufu yake wale hawaisikii wanaona ni kitu cha kawaida kwa sababu kujisaidia katika bidet anaona tusi kwake. Sasa takataka za barabarani yeye akaweke wapi. Hujaona barabara ya Morogoro mzungu anajenga na kusafisha asubuhi ili kesho aweke udongo mzuri anakuta magunia ya taka yamelundikwa katikati pale KAGERA. Watanzania ni wachafu, huko katika mahekalu yanayoshamiri kila siku ukiende usiombe kwenda chooni. Utamaduni wa kutunza choo hana mtu. Usimwone kavaa tai.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...