Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Yanga na Simba itakayochezwa Jumatano (Oktoba 3 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648 kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000.

Mechi hiyo namba 80 ya Ligi Kuu ya Vodacom itachezwa kwenye uwanja huo kuanzia saa 11 kamili jioni. Watazamaji watakaotaka kuona mechi hiyo wakiwa wameketi kwenye viti vya rangi ya bluu ambavyo ni 17,045 watalipa sh. 7,000 kwa tiketi moja.

Viingilio vingine kwenye mechi hiyo ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897 wakati VIP C inayochukua watazamaji 4,060 itakuwa sh. 15,000. Kwa upande wa VIP B tiketi ni sh. 20,000 na VIP A yenye watazamaji 748 tu kiingilio kitakuwa sh. 30,000.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hakuna raha ya Maisha kama kunoa kisu huku ukijiandaa kumchinja mnyama!

    Maana unakuwa na uchu sana kadri muda unavyosogea, ni kama hiyo j5 inayokuja!

    ReplyDelete
  2. Kisu chenye makali kinapozama kwenye koromeo la mnyama, lohhh ni tukio tamu hilo?

    Kuelekea kuchinjwa , mnyama anaweza kuwa na kiburi halafu akaleta usumbufu kidogo, kinachofanyika anafungwa kamba miguuni na wanatafutwa wasaidizi wa kumshika sawasawa ili KISU kifanye kazi yake bara bara!

    Kinachobaki ni mnyama kurusha miguu akivuta pumzi za mwisho baada ya KOROMEO KURARURIWA VIBAYA KWA KISU KIKALI , na hapo 'mnyama' anaondoka rasmi ktk maisha yake matamu akiandaliwa kuliwa supu!

    Hivyo ndivyo Simba mnyama atakavyo zamishwa kisu jumatano!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...