Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh ( kushoto ) akishikana mkono na Mkuu wa Mkoaa wa Morogoro, Joel Bendera ( wapili kushoto) wakati wa kuimba nyimbo ya mshikamano wa wafanyakazi , kabla ya Mkuu huyo wa Mkoa kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi hiyo Sept 10, mwaka huu kwenye ukumbi wa Hoteli ya Morogoro.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya NAOT wakiwa wameshikana mikono wakati wa kuimba nyimbo ya mshikamano wa wafanyakazi , kabla ya Mkuu huyo wa Mkoa kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi hiyo Sept 10, mwaka huu kwenye ukumbi wa Hoteli ya Morogoro.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya NAOT wakimsililiza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( hayupo pichani) wakati akisoma hotuba yake ya kufungua Baraza hilo Septemba 10, mwaka huu katika ukumbi wa Hoteli ya Morogoro.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh ( kulia ) akimkaribisha Mkuu wa Mkoaa wa Morogoro, Joel Bendera ( kati kati ) kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi hiyo Sept 10, mwaka huu kwenye ukumbi wa Hoteli ya Morogoro.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya NAOT wakibadirishana mawazo mara baada ya kupiga picha ya pamoja na Mgeni rasmi , Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( hayupo pichani) alipofungua Baraza hilo Septemba 10, mwaka huu katika ukumbi wa Hoteli ya Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( watatu kutoka kushoto) akifuatiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh walipokuwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la NAOT mara baada ya Mkuu huyo wa Mkoa kulifungua Septemba 10, mwaka huu katika ukumbi wa Hoteli ya Morogoro.Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii,Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Cheki wadada wa dini zote wanavyopendana na kufurahi pamoja.
    Halafu wajinga wachache wanatumia udini kuwabagueni, enyi Watanganyika kuwe makini na umoja wenu, duniani kote hakuna tunu kama hii, aliyoijenga Mwl.J.K.Nyerere.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...