Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi. Claudia Mpangala (kulia) akiwakaribisha ofisini kwake wageni kutoka Malawi na Sierra Leone ambao wako nchini Tanzania kujifunza masuala mbalimbali ya utendaji kazi yanayofanywa na Tume ya Utumishi wa Umma.
Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi. Claudia Mpangala (upande wa kulia katikati) akiwa na baadhi ya watendaji wa Tume ya Utumishi wa Umma akisikiliza maelezo kutoka kwa Bi. Geoigiana Kamara (kulia) kuhusu utendaji kazi wa Ofisi ya Rasilimali watu ya Sierra Leone.
Afisa Tawala Mkuu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Chele Ndaki akitoa maelezo ya namna Tume hiyo inavyotekeleza majukumu yake kwa wageni kutoka Malawi na Sierra Leone ambao wako nchini Tanzania kujifunza masuala mbalimbali ya utendaji kazi yanayofanywa na Tume ya Utumishi wa Umma.
Naibu Katibu wa Idara ya Zimamoto na Uokaji, Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Donarld Ndagula (kushoto) akimsikiliza Bw. Abel Mwamlima kutoka Idara ya Utumishi wa Umma,Sera, Utafiti na Maendeleo kutoka nchini Malawi (aliyeshika kalamu) wakati wa kikao cha pamoja cha kubadilishana uzoefu katika shughuli za utumishi wa Umma kati ya Tanzania,Malawi na Searra Leone.Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.






wafundisheni na namna ya kupokea rushwa maana bongo tunaongoza kwa kupokea rushwa.
ReplyDeleteankali haki ya nani tena unabana comment mpaka watu tunaona uvivu kupoteza muda wetu kwa kuandika au kufungua blog yako.
Kuna watakachojifunza kweli hapa tanzania hawa watu? Hii nchi wachakachuaji niwengi mno haswa katika sekta za serikali. Sijuwi lakini, mhhh!
ReplyDeletekwakweli hawa wamekija kujifunza kutokuwa na ukarimu kazini na kuwa mbabe kwa kila atakaye fika ofisi kwao maana ndo za wabongo ukifika ofisi za serikali. watu walishafanya kama kwa babu yao maana nikisema nyumbani huwa watanzania niwakarimu majumbani kwao, unaanza kukaripiwa na kuonyeshwa sura ya ukali hata ujaeleza unachokiitaji wengene watajifanya wako bize na simu au face_book niwaonea huruma walio tuma watumishi wao kuja kujifunza ubabe kazini.
ReplyDeletethis is the joke of the century. How do you learn corruption? Take the money etc without going to jail - and when u take government money make sure you take a lot. Thats all they can learn from here. The country stinks - it is rotten with corruption. God bless bongo!!
ReplyDeleteHallow mdau uliyesema watz wawafundishe na jinsi ya kupokea rushwa...hao ndio wenyewe wesr african countries zooote, sisi labda tupewe somo la rushwa kutoka kwao.. By the way rushwa ni kila mahala. Cha muhimu wajifunze customer service kutoka kwetu angalau kidogooo tunajitahidi kwakuwa tuna lugha laini ukilinganisha nao utafikiri wanaugomvi na mtu....michuzi najuwa huwezi bana comment yangu...Tanzania hoyeeeee....mdau new york, KKK oyeee
ReplyDelete