Mkurugenzi wa mfuko wa jamii wa LAPF Eliud Sanda katikati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mkutano wao watano wa wadau wa mfuko huo wa jamii unaotarajiwa kuanza kesho katika ukumbi wa mikutano wa AICC jijini arusha wa kwanza kulia ni mkutugenzi wa wa huduma kwa wanachama Valerian Mablangeti (picha zote na woinde shizza,Arusha. Picha na Habari na Woinde Shizza wa Globu ya Jamii, Arusha
ZAIDI ya wanachama 400 wa mfuko wa jamii wa LAPF pamoja na wadau
mbalimbali wa mfuko huo wanatarajiwa kuuthuria mkutano wa tano wa mfuko huo
unatarajiwa kufanyika jijiji Arusha .
Akiongea na waandishi wa habari mkurugenzi wa mfuko huo Eliud Sanga alisema
kuwa mkutano huo ni watano kufanyika tangu kuanzishwa kwa mfuko huo na hii ni
mara ya kwanza kufanyika jijini Arusha.
Alibainisha kuwa zaidi ya wanachama 400 wanatarajiwa kushiriki mkutano
huu pamoja na wadau mbalimbali wa mifuko ya jamii wakiwemo wa ndani ya nchi
pamoja na nje ya nchi huku akibainisha nchi mbalimbali zinazoshiriki mkutano
huu ni pamojna na wadau wa mifuko ya jamii kutoka nchi za zilizopo katika
jumuiya ya Afrika mashariki ambapo alitaja kuwa ni pamoja na kenya ,uganda
,burundi Rwanda na zambia.
Alisema kuwa kwa Apa watu wengine ambao watashiriki na wamealikwa katika
mkutano huu ni pamoja na shirika la nyumba tanzania halimashauri vingozi
wa halimashauri zote hapa nchini ,meya wa halmashari zote ,makatibu
tawala pamoja na mifuko mingine ya kijamii.
Alisema kuwa katika mkutano huu kutakuwa na mada mbalimbali ambazo zitajadiliwa
na washiriki ikiwemo mchango wa mifuko hii ya hifadhi ya jamii, Nafasi ya
mufuko wa jamii ,kujiandaa kustaafu pamoja na kuwapa washiriki elimu kuhusiana
na ugonjwa wa saratani.
Alisema leongo la mkutano huu ni kupanua wigo wa maoni pamoja na mawazo ya
wananchama huku akibainisha kuwa kauli mbiu ya mkutano huu kwa mwaka hu ni
hifadhi ya jamii na ukuaji wa uchumi,
Alisema kuwa mkutano huu utafanyika kwa siku mbili ambapo alibainisha kuwa
unatarajiw akufunguliwa na waziri wa tamisemi ofisi ya waziri mkuu na kufungwa
na rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...