Naibu Waziri wa Katiba
na Sheria Mh. Angellah Jasmine Kairuki akipata maelezo kutoka
kwa Kaimu Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mh. Jaji Mmila alipofanya
ziara ya kikazi leo ya kutembelea baadhi ya Mahakama nchini
ikiwemo Mahakama Kuu ya Tanzania, Mahakama ya Mwanzo Kimanzichana, Mahakama ya
Wilaya Kisarawe na Mahakama ya Mwanzo Kibaha Maili Moja.
Hakimu Mkazi
Mwandamizi Mfawidhi wa Wilaya ya Mkuranga Mh. Abdala A. Pendekezi (wa pili
kulia) akimwonesha kiwanja kitakachojengwa Mahakama ya Mwanzo
Kimanzichana Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Jasmine
Kairuki (wa kwanza kulia) alipofanya Ziara ya Siku moja ya kutembelea
Mahakama nchini. Wa kwanza Kushoto waliosimama mbele ni Naibu MKurugenzi wa
Mahakama za Mwanzo Mh. Warsha Numbu, anayefuatia nI Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga
Mh. Mercy Sila.
Jengo jipya la
Mahakama ya Wilaya ya Kisarawe lililopo Kisarawe mjini Mkoani Pwani. Jengo hili
ni la kisasa ambalo lina korti mbili, mahabusu ya wanawake na ya wanaume, vyoo
vya ndani na nje, stoo na ofisi mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...