Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi linawahamasisha Watanzania wajitokeze kwa wingi kwenda kumshangilia Francis Cheka katika mpambano wake na Benjamin Simon wa Ujerumani.

Mpambamo huo ambao utafanyika tarehe 18 November 2012 katika ukumbi wa Universal jijini Berlin nchini Ujerumani utawakutanisha miamba miwili iliyosheheni kila aina ya ujuzi wa kupigana.

Watanzania wawe na tabia ya kuwaenzi wenzao wanapowakilisha taifa hili kama wenzetu wa nchi nyingine kama Kenya na Uganda wanavyofanya.

Mbali na watanzania watakaokwenda wakifuatana na Francis Cheka tokea nyumbani, pia watanzania wanaoishi nchini Ujerumani na nchi nyingine za Ulaya kama Uingereza, nchi za Skandinavia, Ufaransa, Uholanzi, Hungary na nyingine wanaombwa kujitokeza kwa wingi ili waweze kumshangilia Mtanzania mwezao aweze kupeperusha bendera ya nchi yetu vizuri.

Tayari mtangazaji maarufu wa ITV na Radio One “Maulid Baraka wa Kitenge” pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Jambo Concept inayomiliki magazeti ya Jambo Leo, City Sports Lounge, Jambo Magazine Brand Tanzania bwana Juma Abbas Pinto aliye pia mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) wameshaonyesha nia ya kwenda Ujerumani kulitangaza pambano hilo kwenye vyombo vyao vya habari pamoja na kumshangilia Francis Cheka.

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) inahamasishwa pia itumie nafasi hii kuitangaza nchi yetu huko Ulaya kama zinavyofanya bodi nyingine kama za Kenya, Botswana, Uganda, Oman na nyinginezo zinazotumia wanamichezo wake kutangaza vivutio vya kitalii nchini mwao.

“Tunaishauri Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) izitumie nafasi ambazo watanzania wanawakilisha nchi ili kutangaza vivutio vyake vya katalii”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kwenda Ujerumani.

    Tatizo Waandaaji ni suala la visa hawa jamaa Ubalozi wanawalalia sana watu huku ikieleweka kuwa kwa Mtanzania mwenye akili kwamwe hawezi 'KUZAMIA' huko Ujerumani kwa kuwa kwa sasa Afrika ndio Ulaya ya sasa!.

    Hao Wazungu wenyewe wenye akili nzuri imekuwa kinyume chake kwa sasa wanahamia Afrika!

    ReplyDelete
  2. Unayo sema ukweli sasa Afrika ndiyo imekuwa Ulaya. Kila mara nina kuta watu wana niambia kwamba wameshafika Tanzania. Wako Wamerikani wamenunua ardhi na kujenga nyumba na wana ishi huko. Wegenewe wana ishi kwenye kisiwa cha Mafia. Wengenewe wame owa wakina mama waTanzania. Wako Merikani wengi wanao ishi Tanzania. Hakuna kazi huku wana kimbia Afrika.Tuna danganya sisi tusiwe na haki ya kurundi kwetu.

    ReplyDelete
  3. haha ha ha !!! wewe mtoa maoni,kweli unajua fika kwamba africa imekuwa ulaya, ila waafrica walioko huko majuu bado wamelala kwa maana hiyo wanaifikiria africa ya leo ni kama ile ya enzi za kina Idd Amini au enzi za UDA, wakati kariakoo kulikuwa na nyumba za nyasi, na hawa mabalozi wa mataifa ya nje wao ndo kabisaa, hata kama nchi zao zimegeuka ombaomba kwa mchina lakini hawaoni wala hawasikii kwamba mpira ,upepo umewageuka . Zebedayo msema kweli.

    ReplyDelete
  4. Ahaaaa Zebedayo, kweli naona kuna jamaa toka majuu alikimbia na demu wako, maana umewaandama sana. Pole. Jipange tu. Kwenye ishu iliyopita, ya mwanamke aliyepotea, unaongelea jamaa wa ughaibuni na hapa napo vile vile, duh! Siwezi hata kukujibu bali kukupa pole sana. Wabongo wataingia na kutoka na hapo hamna kitu kinachokupa wewe au kukupunguzia haki zaidi ya mwingine. Endelea kutapatapa tu. Maisha mdundo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...