Mjumbe wa Kamati Kuu ya NEC,Rais wa Zanzibar,Dk. Ali Mohamed Shein akimpongeza Khamis Sadifa Juma, baada ya kutangazwa Mshindi wa kuwa Mwenyekiti mpya wa UVCCM Taifa, katika uchaguzi uliofanyika jana mjini Dodoma.
Aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM,Beno Malisa akimpongeza Khamis Sadifa Juma, baada ya kutangazwa kuwa Mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti mpya wa UVCCM Taifa, katika uchaguzi uliofanyika jana mjini Dodoma.Kulia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya NEC,Rais wa Zanzibar,Dk. Ali Mohamed Shein.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya NEC,Rais wa Zanzibar,Dk. Ali Mohamed Shein akiwa na Mwenyekiti mpya wa UVCCM, Khamis Sadifa Juma na Makamu Mwenyekiti mpya wa UVCCM, Mboni Mhita baada ya viongozi hao wapya wa Umoja huo kutangazwa kuwa washindi leo katika uchaguzi mkuu wa UVCCM uliofanyika jana mjini Dodoma.
Kamanda wa Chipukizi Taifa,Kingunge Ngombale-Mwiru akijadili jambo na Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama wakati wa kutangazwa matokeo. Picha na Bashir Nkoromo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hv umoja huu wa UVCCM ulishawahi kuna na Mwenyekiti Mwanamke?...Vijana wa CCM mi nawatakia kila la heri na tunategemea mabadiliko toka kwenu na sio malumbano..

    ReplyDelete
  2. Baadhi ya sifa za wazanzibari ni uadilifu, uaminifu na ukweli. Hizi sifa zote anazo na ndio zilizopelekea watu wa jimbo la Donge kumpa ubunge. Lililo muhimu ni Sadifa kuwaunganisha vijana wa kada zote katika kukisafisha chama na kutetea maslahi ya wanyonge.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...