Maafisa
wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama hapa nchini pamoja na Mamkala ya Bandari
Zanzibar, wamefanya oparesheni maalum ya ukaguzi wa meli ya AZAM Sealink -1iliyoingia
nchini juzi kuangalia kama ina ubora na kukidhi vigezo vya usafirishaji wa
abiria na mizigo majini yakiwemo magari.
Maafisa waliofanya ukaguzi huo ni
kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi, Usalama wa
taifa, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Mamlaka ya Usalama Bandarini na
Huduma za Meli Zanzibar (ZMA) na Mamlaka ya Usafiri wa nchi Kavu na
Majini (SUMATRA).
Pamoja na kuangalia ubora na vigezo
vingine, Maafisa hao pia wamepata maelezo toshelezi juu ya ubora wa meli hiyo
kutoka kwa Kampuni ya RFI iliyopewa dhamana ya kuisafirisha
Meli hiyo kutoka nchini Ugiriki hadi hapa nchini.
Akizungumza na Ujumbe huo ndani ya
Meli hiyo iliyoweka nanga nje kidogo ya Bandari ya Zanzibar, Mkurugenzi wa RFI
Bw. Stefan Nedkoff, alisema kuwa meli hiyo imeweza kusafiri yenyewe kutoka
nchini Ubeligiji hadi hapa nchini pasipo msaada wowote wa kiufundi.
Amesema kuwa katika maeneo
waliyopitia walipambana na kila aina ya dharuba na kuvuka vikwazo vya mikondo
mikubwa ya bahari kwenye kina kirefu na Meli hiyo iliweza kuhimili hali hiyo.
Alisema Meli hiyo inayoongozwa kwa
mifumo ya kompyuta, ina uwezo mkubwa wa kuhimili misukosuko ya hali ya bahari
na kusafiri umbali na kina kirefu cha maji baharini pasipo shaka.
Bw. Nedkoff amesema kuwa, mbali ya
kuwa meli hiyo ilisafiri ikiwa tupu, lakini itahimili vishindo zaidi vya
baharini pale itakapokuwa na abiria na mizigo ya kutosha.
Amesema kuwa mbali ya uwezo wake wa
kubeba abiria 1,500, lakini pia meli hiyo inauwezo wa kuchukua mizigo yakiwemo
magari 200 kutoka eneo moja kwenda jingine vyote vikiwa na uzito wa tani 500
bila ya kuwa na tatizo lolote la kiusalama.
Maafisa walioitembelea meli hiyo,
wameonyeshwa njia maalum za kujiokolea pamoja na vifaa muhimu vya kiusalama
vinavyoweza kutumika kwa uokozi wakati itokeapo ajali majini.
Meli hiyo pia ina vitanda vya kutosha
kwa ajili ya wagonjwa na abiria watakaojisikia kupumzika wakati wanapokuwa
safarini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari
mjini Zanzibar mara baada ya kuwasili kwa Meli hiyo, Meneja Mkuu wa Kampuni ya
Azam Coastal Ferry inayomiliki Boti ziendazo kasi za Kilimanjaro, Bw. Hussein
Mohammed Saidi, alisema meli hiyo itafanya safari zake kati ya Dar es Salaam,
Zanzibar na Pemba.
Amesema Kampuni yake ambayo ipo
kihuduma zaidi, pia itaangalia uwezekano wa kuweka viwango vya nauli
itakayomfanya kila mtu kusafiri yeye pamoja na jamaa ama watoto wake bila ya
kujinyima.
Bw. Hussein alisema watoto wenye umri
wa kuanzia saa moja hadi mika mitano watasafirishwa bure na wanafunzi watatozwa
nusu ya nauli ya mtu mzima kwa kila safari.



Ukaguzi siyo issue.. Tatizo ni tamaa ya Pesa kwa kupakia abiria wengi zaidi ya uwezo wa Meli.
ReplyDeletehii ni meli au ferry/panton jamani?
ReplyDeleteHivi ajali inapotokea utaanzia wapi kulaumu au chombo gani kinastahili kuwajibika,kwa sababu naona hapo kila mmoja ni mkaguzi.Imefika mahala tupate chombo kimoja cha uchaguzi badala kushirikisha kila mtu.
ReplyDeleteHii ni Panton sio meli
ReplyDelete