Bendi ya Mashauzi Classic “Wakali wa Kujiachia” kesho  (Ijumaa) itatambulisha albam yao mpya wakati watakapo tumbuiza katika ukumbi wa Da West Park, Tabata. Onyesho hilo limedhaminiwa na Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi.
Mratibu wa onyesho hilo Joseph Kapinga amesema kuwa itakuwa ni nafasi pekee kwa wakazi wa Tabata na vitongoji vyake kushuhudia utambulisho wa albamu hiyo liitwayo “Viwavijeshi.”
Bendi hiyo inayoongozwa na mwanadada Isha Mashauzipia inatamba na baadhi ya nyimbo kama Si Bure Una Mapungufu, Anayejishuku Hajiamini, Niacheni Nimpende", Mama Nipe Radhi, Nani Kama Mama na Tugawane Ustaraabu .
Mwimbaji nyota wa kundi hicho, Aisha Othman 'Mama Vuvuzela' pia ataimba wimbo wake mpya uitwao, La Mungu Halina Mwamuzi .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...