Mhe. Hamad  Rashid Mohamed akitoka katika mkutano na  Mwenyekiti wa kamati ya maswala ya Ulinzi na Usalama wa kimatifa Mhe. Saber Chowdury kutoka Bangladesh mara baada ya mjadala huo. Mbunge huyo wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano wa Chama cha Mabunge Duniani  ameteuliwa na kamati tendaji ya chama cha Mabunge duniani (IPU) kuwa mjumbe wa kamati ndogo ya ukaguzi wa ndani kwa mahesabu ya mwaka 2013 ya chama hicho.
Uteuzi huo ulifuatia pendekezo la umoja wa Mabunge ya Afrika lililowasilishwa na katibu mkuu wake Koffi N’Zi tarehe 22 Oktoba, 2012 kufuatia kikao cha wajumbe wa umoja wa Mabunge ya Afrika kumchagua Mhe. Hamad kuwakilisha Afrika kuwania pendekezo hilo mbele ya kamati tendaji ya chama hicho.
 Mhe. Hamad  Rashid Mohamed akitoka katika mkutano na  Mwenyekiti wa kamati ya maswala ya Ulinzi na Usalama wa kimatifa Mhe. Saber Chowdury kutoka Bangladesh mara baada ya mjadala huo
Mbunge kijana kutoka Afrika Kusini Mhe. Judith Tshabalala akichangia kwa hisia kali tatizo la ajira kwa vijana na jinsi mabunge mengi duniani ambavyo  hayajalivalia njuga swala hili: 
 
Mjumbe wa Tanzania katika mjadala wa Wabunge Vijana kujadili na namna ya kupunguza ajira kwa vijana hususani katika kipindi hiki cha uchumi wa utandawazi uliondoandaliwa na Chama cha Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika Mkutano wake Mjini Quebec, Canada, Mhe David Kafulila akinyoosha karatasi kupeleka ujumbe wa kuchangia katika mjadala huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...