Rais Jakaya Mrisho kikwete na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda wakipitia Waraka wa Utumishi Namba 5 wa mwaka 2009 kuhusu matumizi bora na salama ya vifaa na mifumo ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA) serikalini wakati wa kikao cha kazi (retreat) cha siku tatu cha Mawaziri, Manaibu Mawaziri na maafisa waandamizi wa serikali kujadili mikakati endelevu na utekelezaji wa sasa na wa baadae katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha kazi (retreat) cha siku tatu cha Mawaziri, Manaibu Mawaziri na maafisa waandamizi wa serikali wanaokutana kujadili mikakati endelevu na utekelezaji wa sasa na wa baadae katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma. Pamoja naye meza kuu ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali (kulia) na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...