Katika toleo ya Jumatatu wiki hii la Globu ya Jamii na  blogu nyingine  ilitolewa habari iliyokuwa na kichwa cha   ‘TANZANIA KUONDOKA KATIKA KUNDI LA NCHI MASKINI IFIKAPO 2015’

Habari ile ilikuwa na kosa la kiuandishi  kwenye eneo la mwaka, ukweli ilikuwa isomeke  Tanzania   inatarajiwa kuondoka kwenye kundi la nchi maskini  na kuwa nchi yenye Uchumi wa Kati ( Middle Income Country) ifikapo mwaka2025 na si 2015.

Mwandishi  wa habari  ile na ambayo ilimnukuu Naibu  Katibu  Mkuu Mtendaji  Ofisi ya Rais  Kamisheni ya Tume ya Mipango, Bw. Clinfford K. Tandari  (pichani juu)   anachukua  fursa  hii kumwomba  radhi  Mhusika  Mkuu wa habari ile   kwa  usumbufu wowote alioupata na pia anawaomba radhi wadau wengine ambao kwa namna moja ama nyingine  walikwazika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. will all those angry, rightfully so, commentors be apologizing?

    ReplyDelete
  2. Kuna waziri wetu Hon Philipo Augustino Mulugo, Dep Min of Education & Voc Training nae aliitangaza Zimbabwe kuwa imo katika muungano wa Tanzania inabidi nae tupate sahihisho lake hapa. Angalia hotuba yake hapa http://www.youtube.com/watch?v=e3BNegmIUKM&feature=share

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...