Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Swaziland,Mh. Joseph Ndallah (pili kushoto) akimkabidhi Balozi Mstaafu wa Tanzania nchini Swaziland,Mhe. Pastor Ngaiza zawadi iliyoandaliwa na Wanajumuiya ya Tanzania waishio Swaziland siku walipomuaga rasmi kwenye Ukumbi wa Manzine Portuguese Club. Kwa sasa Mhe. Ngaiza yupo nchini Tanzania baada ya kustaafu rasmi utumishi wa Umma. Aidha Watanzania wa Swaziland hapo awali hawakuweza kumuaga na walitumia wasaa wa kumuaga baada ya Mhe Ngaiza kupita nchini Swaziland katika ziara binafsi. Watanzania wote wanampongeza Mhe. Ngaiza kwa kazi nzuri aliyoifanya ya uwakilishi wa nchi yetu kwenye nchi za Mozambique, Swaziland, Comoros na Madagascar hadi alipostaafu. Tunamtakia maisha mema: Imewasilishwa na Watanzania wote waishio Swaziland.
Katibu Mstaafu wa Jumuiya ya Watanzania Swaziland,Bi. Juliet Mgonda akiongea machache kabla ya kumkaribisha,Mwenyekiti aliyemaliza muda wake,Mama Mwanaisha Kaoya. Mama Kaoya ambaye ameketi na kupozi kwa kilemba kilichoenda shule. Wote walihudhuria hafla ya kumuaga Balozi Mstaafu Mhe. Pastor Ngaiza.
Wanajumuiya wakimtakia maisha mema Mhe. Pastor Ngaiza, Balozi Mstaafu kwa kugonganisha glasi kuashiria pongezi kwa Mhe. Ngaiza baada ya kustaafu utumishi wa umma salama.
Picha ya Pamoja: Balozi Mstaafu,Mhe. Pastor Ngaiza (katikati) akiwa na kushoto kwake ni Dr. David Polepole, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Swaziland, Bw. Joseph Ndallahwa, Balozi wa Heshima wa Tanzania - Swaziland; Bw. Jonas Tunzo - Katibu wa Jumuiya ya Wanzania Swaziland; Bw. Patric Lwabukuna, Mjumbe wa Jumuiya anayewakilisha eneo la Matspha; Bw. Juma Ngalahwa, Mjumbe wa Jumuiya - Manzini; Kulia kwa Mhe. Balozi ni Bw. Frank Mwega - Afisa wa Ubalozi wa Tanzania, Maputo Mozambique; Bi. Agnes Ngonyani, Mjumbe wa Jumuiya - Mbabane na Bi. Hadija Michel Mtunza Hazina wa Jumuiya.
Mhe Pastor Ngaiza, Balozi Mstaafu wa Tanzania nchini Mozambique, Swaziland, Comoros na Madagascar akiwa kwenye picha ya pamoja na Watanzania waishio nchini Swaziland, walipofanya sherehe rasmi ya kumuaga tarehe 20 Oktoba, 2012 katika ukumbi wa Portuguese Manzini Club, Manzini - Swaziland. Kushoto kwa Mhe. Balozi ni Dr. David Polepole, Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Watanzania; Bw. Joseph Ndallahwa, Balozi wa Heshima wa Tanzania Swaziland; Kulia kwa Mhe. Ngaiza ni Bw. Frank Mwega, Afisa wa Ubalozi wa Tanzania, Maputo - Mozambique na Mama Mwanaisha Kaoya, Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya Watanzania na Watanzania wengine.


thanks for those who attended we have continue with our faith.Thanks for Ngaiza for visiting us.Jones
ReplyDeleteThat was really nice, paying a ferewell to someone who represented our nation in a very respected way! We'll always remember you Hon. Ngaiza.
ReplyDeleteOur sincere appreciation to those who attended and those who prepared the event..... Big-up
Juma Ngallawa