Balozi Dora Msechu akichangia majadiliano kuhusu ajenda ya uwezeshaji wa wanawake wakati wa mkutano wa Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la 67 la Umoja wa Mataifa, katika mchango wake, Balozi Dora Msechu alizungumzia juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali katika kukomboa mwanamke na mtoto wa kike dhidi ya vitendo vya kikatili, unyanyasaji na ukosefu wa huduma za kuridhisha za huduma ya afya ya mama mjamzito. Aidha katika mchango wake, Balozi Msechu amesisitiza haki na fursa ya wanawake kushiriki katika majadiliano ya kutafuta amani ili kuifanya dunia kuwa mahali salama.
Rais wa Baraza Kuu la 67 la Umoja wa Mataifa, Bw. Vuc Jeremic ambaye ameahidi kufanya kazi kwa Karibu na Kamati ya Tatu ya Baraza hilo inayohusika na masuala ya Maendeleo ya Jamii, Haki za Binadamu na Utamaduni katika kusukuma mbele ajenda zinazohusu maendeleo ya wanawake, fursa sawa za kijinsia na uwezeshaji.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...