Uongozi wa
Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) unapenda kuwataarifu Wateja na Wananchi wa Dar es Salaam
kwa ujumla kuwa taarifa iliyotolewa na Gazeti la kila siku la Mwananchi toleo
la siku ya Jumanne Oktoba 02, 2012 kwamba SUMATRA
ndiyo kikwazo cha kuanza kwa huduma ya usafiri wa treni jijini Dar es Salaam
siyo sahihi.
Katika mchakato
wa kutoa huduma za usafiri wa treni
ambayo hapo awali haikuwepo jijini, wadau wa kufanikisha mradi huu ni taasisi nyingi ambazo zinapaswa kuchangia
kuanzishwa kwake. Hivyo basi mchakato huo ni wa lazima na
hakuna njia ya mkato . Tunapenda kueleza wazi kuwa siyo sahihi kusema kuwa TRL imekwama kuanza
kutoa huduma ya usafiri wa treni ya
abiria jijini kutokana na SUMATRA kutoidhinisha viwango vya nauli na
kutopewa leseni.
Uongozi
wa TRL unapenda kutoa rai kwa Waandishi habari na Wahariri wao kabla ya
kuchapishwa habari nyeti kama hii inayogusa maslahi ya Wadau wengi na hasa wale
wanaongojea kwa hamu huduma hii ianze kujitosheleza kuwa habari wanayoichapisha ni sahihi na kama
inajenga au kubomoa.
Ukweli ni kwamba TRL hivi sasa inakamilisha
mchakato wa kuandaa na kuwasilisha
vigezo ambavyo vinahitajika na SUMATRA ili
iweze kufanya tathmini yake na hatimaye kutoa leseni ya huduma ya treni jijini
.
Tunarudia Uongozi
wa TRL unasikitika kwa usumbufu uliotokana na taarifa hizo zisizo sahihi kwa
Wadau wote na hasa kwa Uongozi wa SUMATRA.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa
Niaba ya Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa TRL
Mhandisi Kipallo A. Kisamfu
Dar es salaam,
Oktoba 2, 2012
TWATAKA VITENDO,Maneno sasa yanachosha!
ReplyDeleteMnaaaaaanza sasa Kugongana kweli Bongo Tambarare kweli Msemo wa USITOE AHADI WAKATI WA FURAHA NDIO HUO watu wamesubiri kwa Hamu sasa mvutano jaribuni jamani kujirekebisha WANANCHI WAPATE USAFIRI NA HIZO FENI MSIJE KUZITOA TU. M
ReplyDeleteTreni hizi ni za kizamani sana. Sijui kwa nini tunaringa nazo. wenzetu walizitumia miaka ya 1960.
ReplyDeletetutafika katua ndogo ndogo.
BS...kumbe hamjajipanga sasa mbona mlituambia mwezi wa kumi? Hizi longo longo zitaisha lini Bongo? Jipangeni kwanza alafu ndio mtuambie lini mtaanza hii kitu.
ReplyDeleteSuala hili ni la umuhimu mkubwa na pia linawagusa wananchi wengi wa kipato cha kawaida. Sitegemei na wala sipendi siasa katika hali. Taratibu zikamilike haraka ili wananchi waanza kutumia huduma ya treni na kuondokana na adha ya usafiri dar japo kidogo.
ReplyDeleteFanyeni utafiti wa kutosha kabla kutoa ahadi zisizo tekelezeka.
ReplyDelete
ReplyDeletehahaha kazi kweli kweli me naona jamani imefika hatua sasa tunatakiwa kumuita raisi ya rwanda aje awe wa Tanzania angalau kwa mwaka 1