TUNAPENDA KUWAFAHAMISHA WASAFIRI WETU WA RELI YA KATI DARAJA LA TATU KWAMBA, KUANZIA SASA WATOTO WA UMRI CHINI YA MIAKA SABA WATASAFIRI BURE NA WATAPEWA KITI/VITI.

 WATOTO HAO WATATAKIWA KUSAFIRI NA WAZAZI/WALEZI WAO NA PIA WAJE NA VYETI VYA KUZALIWA AU BARUA YA SERIKALI YA MTAA HUSIKA KUTHIBITISHA UHUSIANO NA MZAZI/MLEZI WAKE. 

MZAZI/MLEZI ATAKAYESAFIRI NA WATOTO HAO ATARUHUSIWA WATOTO WASIOZIDI WAWILI KWA WAKATI MMOJA NA NILAZIMA AJE NA VITHIBITISHO HIVYO WAKATI WA KUNUNUA TIKETI YAKE NA AWAANDIKISHE KWA KARANI/STESHENI MASTA ILI WAWEZE KUPATA TIKETI ZA KUSAFIRIA. 

MTOTO ATAKAYEKUTWA NDANI YA TRENI BILA TIKETI ATALIPIA NUSU NAULI YA MTU MZIMA. TUNAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI KUBORESHA HUDUMA HII. 

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano  kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa TRL 
Mtendaji Mhandisi Kipallo A.Kisamfu 
Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Vizuri, wapate viti kwa uhakika, na wakilaghaiwa ama kutishwa ili wapishe viti hatua kali zichukuliwe dhidi ya mafedhuli watakaofanya hivyo.

    Nikiwa mdogo huko mikoani nilisafiri kwa tabu na mateso sana sana. Mtoto wa miaka saba ama nane unatoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine unaambiwa upishe kiti! Na mtu mzima, bila ya aibu, anakaa na kukutazama tu ukiwa unang'ang'ania kutafuta sehemu ya kushika ili usianguke maana juu hufikii na watu wamejaa.

    ReplyDelete
  2. SiKILIZENI KWA MAKINI NA HIZO TICKET MNAZOAHIDI MSIPOZITOWA TUTAKUJA KULALAMIKA HUMU HUMU KAMA MNAVYOJIJENGEA SIFA HUMU ALAFU AHADI AZITIMII.

    ReplyDelete
  3. mimi sijapenda je kama unawatoto watano huwezi kusafiri kwasababu sheria ni watoto wawili hii kali rekebisheni hichi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...