Mwenyekiti wa Tume Ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora Jaji Kiongozi (Mstaafu) Amiri Ramadhan Manento (katikati) akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani jijini Dar es Salaam Oktoba 10,2012 wakati akitoa muhtasari wa taarifa ya Uchunguzi wa Tume yake kuhusu tukio lililopelekea kifo cha Daudi Mwangosi kilichokea Septemba 2, 2012 kijijini Nyololo. Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mahfoudha.A. Hamid na kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Tume hiyo Florida Kazora.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Jaji Kiongozi (Mstaafu) Amiri Ramadhan Manento akionyesha taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu Muhtasari wa wa Taarifa ya tume yake ya Uchunguzi wa tukio lililopelekea kifo cha Mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten Daudi Mwangosi kilichotokea Septemba 2, 2012 kijijini Nyololo, Wilaya ya Mufindi, Mkoani Iringa,.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mahfoudha.A. Hamid akijibu moja ya Swali kutoka kwa Mwandishi wa Habari (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu Muhtasari wa wa Taarifa ya tume yake ya Uchunguzi wa tukio lililopelekea kifo cha Mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten Daudi Mwangosi kilichotokea Septemba 2, 2012 kijijini Nyololo, Wilaya ya Mufindi, Mkoani Iringa.
Waandishi wa Habari wakiwa kwenye ukumbi wa mkutano wa ofisi ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam wakati wa kutoa Muhtasari wa wa Taarifa ya tume yake ya Uchunguzi wa tukio lililopelekea kifo cha Mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten Daudi Mwangosi kilichotokea Septemba 2, 2012 kijijini Nyololo, Wilaya ya Mufindi, Mkoani Iringa.Picha na Mwanakombo Jumaa - MAELEZO.

BOFYA HAPA KUSOMA TAARIFA HIYO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kweli nimeelimishwa kisawa. Mh. Jaji umeonyesha jinsi ulivyobobea ktk taaluma yako,hongera sana! Tunahitaji viongozi kama hawa ktk dunia ya leo. Shukrani kwa taarifa yenye upeo na kina,Mwenyezi Mungu ndie Hakimu Mkuu wa Dunia.

    ReplyDelete
  2. Ripoti nimeipenda imetulia mno,nadhani ndio ripoti inavyotakiwa kuwa pindi panapotokea utata juu ya ukweli kuhusu suala lililotokea.Hongera watoa ripoti kwa kufuata kanuni na taratibu zote ktk kufanikisha ripoti hii.

    ReplyDelete
  3. Taarifa ni ya kisayansi kabisa imefuata ueledi kwani tume yenyewe ilikuwa na wajumbe wenye weledi wa uhakika wamepitia michakato yote ya uchunguzi kupata kiini cha mauaji.

    ReplyDelete
  4. Kumbe hizi tume kazi zao ni kupanga matokeo na kutoa ushindi wa mezani!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...