Afisa Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) Bw. Austin Makani akizungumza na wakazi wa kata ya Pugu akizungumzia kwanini Umoja wa Mataifa katika wiki hii ya maadhimisho ya miaka 67 tangu kuanzishwa pamoja na mambo mengine imeamua kutilia mkazo suala la Utunzaji wa Mazingira kwa kuwa ni moja ya maeneo muhimu unapozungumzia suala zima la kutoa elimu juu ya mabadiliko ya Tabia nchi.
Mtaalamu wa Mazingira na Nishati wa UNDP Dkt. Amani Ngusaro (wa pili kulia) aliyemwakilisha mgeni rasni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini akitoa nasaha zake katika wiki ya maamdhisho ya Umoja wa Mataifa ambapo Umoja huo ulikwenda kufanya kampeni ya kuhimiza wananchi kutunza mazingira katika Kata ya Pugu,
Akizungumza na wakazi hao amewataka kujenga utamaduni wa kupanda miti ikiwa ni pamoja kutunza msitu uliopo katika eneo hilo ambao kwa sasa unaonekana kunyauka na hata kufikia kukimbiwa na wanyama na ndege asili jambo alilosema iwapo hazitachukuliwa hatua za makusudi kuutunza msitu huo utatoweka na kuwa mfano mbaya kwa vizazi vijavyo.
Aidha amesema upo umuhimu wa miradi ya upandaji miti kuwashirikisha zaidi wakazi wa eneo husika na kutaka kampeni kama hizo zishirikishe Tume ya Taifa ya Kuhifadhi Mazingira ili kuweza kutekeleza mikakati ya kutoa elimu juu ya mabadiliko ya tabia nchi kwa ufanisi zaidi.
Muasisi na Mkurugenzi wa Young Tanzanian For Community Prosperity (YTCP) Bw. Alfred Magahema akisalisha mada juu ya umuhimu na njia bora za kutoa elimu kwa Watnzania juu ya mabadiliko ya Tabia nchi ambapo ameshauri elimu hiyo isitolewe mijini tu bali hata katika maeneo yaliyoko nje ya mji pamoja na Vijijini na kuwataka wale wote walioelewa somo hilo wakawe walimu na wahamasishaji kwa wenzao kwa kuwaelekeza umuhimu wa utunzaji Mazangira.
Jovine Malago wa YTCP (kulia) na wakazi wa Pugu wakiwasalishi mapendekezo waliyokubaliana baada ya kufanya majadiliano katika makundi kuhusiana na zipi njia bora zitakazowezesha kuwashirikisha wananchi katika utunzaji wa Mazingira.
Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Pugu Bw. Mlagala akitoa malalamiko ambapo amelizungumzia dampo la Pugu limeathiri wakazi wa eneo hilo ikiwa ni pamoja na kusababisha magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu na pia amezingumzia suala la kukithiri kwa umaskini wa kipato na fikra kuhusiana na utunzaji wa Mazingira na kuuomba Umoja wa Mataifa kupitia miradi yake ya Maendeleo uwasaidie kuwawezesha kuondokana na umaskini kupitia miradi ya ufugaji wa Nyuki na kilimo cha Uyoga.
Mtaalamu wa Mazingira na Nishati wa UNDP Dkt. Amani Ngusaro akipanda mti kwa ajili ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa katika kusheherekea miaka 67 tangu kuanza kwa shirika hilo yenye kauli mbiu "BORESHA MAZINGIRA KWA MAISHA ENDELEVU".
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kinyamwezi Kata ya Pugu Bw. Mohamedi Abdalah akipanda mti kuunga mkono juhudi za Umoja wa Mataifa katika kutunza mazingira wakati wa maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Pugu Bw. Justin Nyangwe akishiriki zoezi la upandaji miti.
Wakazi wa kata ya Pugu katika Picha ya Pamoja na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na vijana wakujitolea wa YTCP baada ya kukamilika kwa zoezi la upandaji miti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa kusheherekea miaka 67.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...