Waziri wa Uchukuzi,Dk. Harrison Mwakyembe akiongozana na baadhi ya viongozi waandamizi kutoka TRC, Mamlaka ya Usafiri wa
Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), TAZARA pamoja na Polisi Kitengo cha
Reli wakati wa uzinduzi wa Safari za Treni ndani ya Jiji la Dar es Salaam mapema leo.
Waziri wa Uchukuzi,Dk. Harrison Mwakyembe akiwa nadni ya treni hiyo sambamba na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi pamoja na viongozi waandamizi kutoka TRC, Mamlaka ya Usafiri wa
Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), TAZARA pamoja na Polisi Kitengo cha
Reli wakati wa uzinduzi wa Safari za Treni ndani ya Jiji la Dar es Salaam mapema leo.
Treni ikiwa safarini.
Abiria
wakiwa ndani ya Usafiri wa Treni huku wengine wakiendelea kupata nyuzz
mbali mbali tena kwa utulivu kabisa kupitia magazeti.
Waoh!
ReplyDeleteTunahitaji nyingine kama 5 hivi kumaliza biashara ya usumbufu wa usafiri. Imagine upuuzi wa matumizi ya fedha nyingi kwenye sijui mabasi ya kwenda kasi zingeenda kwenye reli moja Mbagala, lingine Kibaha, nyingine Tegeta na lingine Pugu!
Je, kufika ama kuondoka kituo cha treni inakubidi upande daladala?
ReplyDeleteNaishukuru sana serikali kwa kazi hii. Hii ni "initiative" nzuri. Sitashangaa baada ya miaka mitatu tukawa na treni ya umeme inayo-shuttle katika jiji la Dar es salaam. Mungu ibariki Tanzania.
ReplyDeleteTreni ya umeme tz chineke, umeme wa maji, au wa mafuta ya taa?
ReplyDeleteGreat Initiative! Hongera sana serikali ya TZ, Hongera Mh. Mwakyembe, tunedelee kuwekeza kwenye miradi kama hii yenye kuleta maendeleo, Tutafika!Mungu Ibariki Tanzania
ReplyDeleteAnon wa 2, hio iko wazi kama kwako ni mwendo kutoka kwenye kituo ulichoshukia utapima aidha utembee au upande daladala lakini ni wazi kabisa utakuwa umepunguziwa usumbufu mkubwa sana wa foleni. Chukulia kuwe na treni Posta - Tegeta na wewe unaenda Boko ukienda na treni hadi Tegeta ndipo ukapandia basi pale huoni utakuwa umeokoa muda na usumbufu mkubwa?
ReplyDeleteNi mwanzo mzuri!
ReplyDeleteAngalau Jiji kwa mara ya kwanza jana limefunguka kwa kupungua shida ya Usafiri.
Tuache ubishi, huu mpango una manufaa sana sana, tulikuwa tunakwamishwa na njia kuu mbili za kutokea katikati ya Jiji hadi Ubungo na hadi Ukonga.
Hongera sana kwa jitihada!
Watu hawajaizoea lakini nafikiri waanze na ruti moja asubuhi na moja jioni ili nao daladala waambulie. Nimeona mwitikio wa abiria si mkubwa. nilitegemea nyomi kama ile ya Jo'burg - soweto
ReplyDeletenimefurahi sana michuzi yaani bla bla zimepungua kama alivyosema mtoa maoni wa kwanza zikipatikana kama tano itakua vizuri.sasa itapatikanaje?inabidi tuanze kujichangisha sisi tulioko nje ya nchi kuonyesha mfano halafu wengine wanafuata kupitia televisiona na radio kurahisish upatikanaji wa treni mpya haraka.au mnasemaje mimi naanza na mchango wa milion 2 wakiongezeka wengine nitaongeza zaidi kadri siku zinavyokwenda.asante
ReplyDeleteLooh! Walitaka kuukatili bure uhai wa Mwakyembe, tungeyaona wapi haya?? Mungu abariki mawazo yako yenye viwango na kuwapa busara washauri wako wote. Huenda jibu la tatizo la usafiri linakaribia kuwa historia baada ya muda mfupi
ReplyDeleteMaendeleo huenda pole pole, anon, twaweza kuwa na Treani ya umeme pia, hii ni mwanzo tu, wa kipiga hatua wangu,
ReplyDeleteNasubiri kuona watu wangapi watagongwa na hizo treni.
ReplyDeleteBei ya Ufisadi tutaiona kwa matunda ya Mhe. Dr.Mwakyembe na jitihada zake.
ReplyDeleteSASA WANDUGU HAYA ALIYOFANYA HAPA NI MFANO WA HAYO YALIYOMGHARIMU MPAKA AKAFANYIWA MPANGO MCHAFU KABISA WA KUHATARISHA UHAI WAKE.
TUUCHUKUIE UFISADI KWA NGUVU ZOTE ILI TUPATE MAENDELEO NCHINI!
Sasa je, BEI GHALI kabisa ya UFISADI hatuioni kwa kuhujumiwa watu wenye mawazo na nia njema kwetu kama Dr.Harrison Mwakyembe???
MUNGU TUSAIDIE KUYAKABILI MAJARIBU!
Huu ni mpango mzuri sana, Naomba uwe endelevu. Nashauri waweke parking ya magari eneo la Ubungo Maziwa ili wenye magari wawe wanayaacha ili wapande treni na wakirudi wanayachukua.
ReplyDelete