Timu ya Watanzania wanaoishi katika mji wa Wichita, Kansas, nchini Marekani, imefanikiwa kuichakaza timu ya watani wa jadi wa Kenya katika mechi iliyochezwa kwenye baridi kali. Ukifanya hesabu za darasa la kwanza za kujumlisha na kutoa, zinaifanya timu ya Watanzania kushinda kwa goli tatu (3) kwa bila (0). Timu ya Timu ya Watanzania inajiandaa kucheza mechi ya marudiano na timu ya Houston Texas, mchezo utakaofanyika Jumamosi ijayo ya tarehe 13, Oktoba, katika jiji la Houston, Texas, nchini humo.
Mshambuliaji hatari wa Tanzania Iddi Ligongo akimtoka beki wa timu ya Kenya.
Hapiti mtu hapa....
Kutoka kushoto walio simama: Juma, Diwani Chehe, Abuusaady Saadiq, Said Saeed, Felix, Deogratias Ngasa, na Idd Ligongo Kutoka kushoto walio chuchumaa Aziz, Ernest, Saleh Kaumbwa, na Denis Rweikiza.





Ligongo hiyo jezi nyekundu imekupendeza sana kaka
ReplyDelete